UTUKUFU SIO KUWA MASHUHURI AU KUWA NA WAFUASI WENGI , BALI UTUKUFU NI KUWA MASHUHURI MBELE YA MOLA WAKO.
Sote tunamjua vizuri sheikh Ally Jaabir , imamu na msomaji qur’aan maarufu lakini hatumjui shekhe wake aliyemfundisha suuratul faatiha .
Twamjua sheikhul islaam ibn Taymiya alivokuwa mashuhuri katika ulimwengu wa kiislamu katika nyanja tofauti tofauti za elimu ya dini na utunzi mzuri wa vitabu lakini hatumjui shekhe wake aliyemfundisha kusoma na kuandika alivokuwa mdogo .
Mwanadamu kuwa mtukufu katika dunia hakuna ulazima wa kuwa mashuhuri kila mmoja akujue , kwani wapo wanaofanya mambo makubwa lakini hawajulikani mbele za wanadamu lakini ni maarufu mbele za MOLA wao .
Imaam Albukhaary , Imaam Muslim , Imam Maalik , Imaam Shaafi , Imaam Swalaahudeen na wengine wote waliandaliwa na watu ambao hawakuwa mashuhuri .
Imam wa msikiti wa haram ya Makkah na Madina pindi wanaposwalisha wanasoma suuratul faatiha na maelfu ya watu wanaitikia “Ameen” lakini hawajulikani walimu wao waliowafundisha suuratul-faatiha lakini ni mashuhuri mbele ya MOLA wao kwa juhudi walizozifanya .
Ni nani aliyemfundisha sheikh Abdulrahman Assumeyt kalima ya Laailaha illaa ALLAH ambayo aliitumia kusilimisha mamilioni ya watu ? hajulikani lakini ni mashuhuri mbele ya MOLA wake .
Je wamkumbuka aliyekuwa wa kwanza kukufundisha Qur’aan , Tawheed , Tafseer na masomo mengine ya dini ? baadhi yao umewasahau lakini ni mashuhuri mbele ya MOLA wao .
Nafasi yako mbele ya MOLA wako sio kwa kutokana na wafuasi wengi au kuwa mashuhuri mbele ya watu , bali utukufu wako ni kuwa mashuhuri mbele ya MOLA wako .
©Abu-Khalfan Assarawi
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. / This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
+255656333678
20 February 2017
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.