Menu

BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


عن ابن عباس ، رضي اللَّه عنهما ، قال : كان عمر رضي اللَّه عنه يُدْخِلُنى مَع أشْياخ بْدرٍ ، فَكأنَّ بعْضَهُمْ وجدَ فِي نفسه فقال : لِمَ يَدْخُلُ هَذِا معنا ولنَا أبْنَاء مِثْلُه ،؟ فقال عمرُ : إِنَّهُ من حيْثُ علِمْتُمْ ، فدَعَانى ذاتَ يَوْمٍ فَأدْخلَنى معهُمْ ، فما رأَيْتُ أنَّه دعانى يوْمئِذٍ إِلاَّ لِيُرِيهُمْ قال : ما تقولون في قول اللَّه تعالى :  { إذا جاءَ نَصْرُ اللَّهِ والْفَتْحُ} [الفتح : 1 ] فقال بَعضُهُمْ : أمِرْنَا نَحْمَدُ اللَّهَ ونَسْتَغْفِره إذَا نَصرنَا وفَتَحَ علَيْنَا . وسكَتَ بعضهُمْ فلم يقُلْ شيئاً فقال لى : أكَذلك تقول يا ابنَ عباس ؟ فقلت : لا . قال فما تقول ؟ قلت : هُو أجلُ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، أعْلمَه له قال : { إذا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ والْفتحُ}  وذلك علامة أجلِك { فَسَبِّحْ بِحمْدِرَبِّكَ واسْتغْفِرْهُ إِنَّه كانَ تَوَّاباً}  [ الفتح : 3 ] فقال عمر رضي اللَّه عنه : ما أعْلَم منها إلاَّ ما تَقُول . رواه البخارى


Kutoka kwa‘Abdullaah bin ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiniingiza katika mashauri pamoja na wazee waliopigana katika Vita vya Badr, basi kana kwamba baadhi yao walihisi kitu moyoni mwao, akauliza: Mbona huyu anaingia pamoja na sisi na wakati sisi tunao watoto kama yeye? ‘Umar akamwambia: Huyu ni kama mnavyomjua! Siku moja akaniita na kuniingiza pamoja nao. Sikuona siku hiyo kuwa ameniita ila ni kwa ajili ya kutaka kuwaonesha wao. Akawauliza: Mnasemaje kuhusu Neno lake Mwenyezi Mungu  [Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,]  Baadhi yao walisema: Tumeamriwa tumuhimidi Mwenyezi Mungu na tumuombe msamaha Atakapotunusuru na Kutupa ushindi. Baadhi yao walinyamaza wala hawakusema kitu. Akaniuliza: Nawe unasema hivyo hivyo Ewe Ibn ‘Abbaas? Nikamjibu: Hapana. Akasema: Unasemaje? Nikamwambia: Hayo ni mauti ya Mtume ﷺ, Mwenyezi Mungu Alimjulisha Akamwambia: [Pindi itakapokuja Nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi.] Hiyo ndiyo alama ya mauti yako, [Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba]     [Surat AnNas'r]

‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Hivyo ulivyosema ndivyo ninavyojua. [Imepokewa na Bukhari]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6573023
TodayToday1090
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 41

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682871c75da9315712834261747481031
title_682871c7721c620635950571747481031
title_682871c77233110955094111747481031

NISHATI ZA OFISI

title_682871c78bc764473539551747481031
title_682871c78bd5f3228581101747481031
title_682871c78be469839578731747481031 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 11 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com