Menu

BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


وعَنْ زِرِّ بْنِ حُبْيشٍ قَال : أَتيْتُ صفْوانَ بْنِ عسَّالٍ رضِي الله عنْهُ أَسْأَلُهُ عن الْمَسْحِ عَلَى الْخُفَّيْنِ فقال : مَا جَاءَ بِكَ يَا زِرُّ ؟ فقُلْتُ : ابْتغَاءُ الْعِلْمِ ، فقَال: إِنَّ الْملائِكَةَ تَضَعُ أَجْنِحتِها لِطَالِبِ الْعِلْمِ رِضاء بمَا يَطلُبُ ، فَقلْتُ : إِنَّه قدْ حَكَّ في صدْرِي الْمسْحُ عَلَى الْخُفَّيْنِ بَعْدَ الْغَائِطِ والْبوْلِ ، وكُنْتَ امْرَءاً مِنْ أَصْحاب النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَجئْت أَسْأَلُكَ : هَلْ سمِعْتَهُ يذْكرُ في ذَلِكَ شيْئاً ؟ قال : نعَمْ كانَ يأْمُرنا إذا كُنا سفراً     أوْ مُسافِرين أَن لا ننْزعَ خفافَنا ثلاثة أَيَّامٍ ولَيَالِيهنَّ إِلاَّ مِنْ جنَابةٍ ، لكِنْ مِنْ غائطٍ وبْولٍ ونْومٍ . فقُلْتُ : هَل سمِعتهُ يذكُر في الْهوى شيْئاً ؟ قال : نعمْ كُنَّا مَع رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم في سفرٍ ، فبيْنا نحنُ عِنْدهُ إِذ نادَاهُ أَعْرابي بصوْتٍ له جهوريٍّ : يا مُحمَّدُ ، فأَجَابهُ رسولُ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم نحْوا مِنْ صَوْتِه : «هاؤُمْ» فقُلْتُ لهُ : وَيْحَكَ اغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ فإِنَّك عِنْد النَّبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وقدْ نُهِيت عَنْ هذا ، فقال : واللَّه لا أَغضُضُ : قَالَ الأَعْرابِيُّ : الْمَرْءُ يُحِبُّ الْقَوم ولَمَّا يلْحق بِهِمْ؟ قال النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : «الْمرْءُ مع منْ أَحَبَّ يَوْمَ الْقِيامةِ » فما زَالَ يُحدِّثُنَا حتَّى ذكر باباً من الْمَغْرب مَسيرةُ عرْضِه أوْ يسِير الرَّاكِبُ في عرْضِهِ أَرْبَعِينَ أَوْ سَبْعِينَ عَاماً. قَالَ سُفْيانُ أَحدُ الرُّوَاةِ  قِبل الشَّامِ خلقَهُ اللَّهُ تعالى يوْم خلق السموات والأَرْضَ مفْتوحاً لِلتَّوبة لا يُغلقُ حتَّى تَطلُعَ الشَّمْسُ مِنْهُ »    رواه التِّرْمذي وغيره وقال : حديث حسن صحيح


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Kutoka kwa  Zirru bin Hubaysh amesema: “Nilimuendea Swafwaan bin ‘Assaal Radhi za Allah ziwe juua yake  nikimuuliza kuhusu kupangusa juu ya khuffu mbili. Akaniuliza: Ni jambo lipi limekuleta Ee Zirru? Nikasema: nimekuja kutafuta elimu akasema: “Hakika Malaika humuwekea mbawa zao mwenye kutafuta ‘Elimu kwa kumridhia anachokitafuta. Nikamwambia: “Kwa hakika nimeingiwa na shaka moyoni mwangu na kupangusa juu ya khofu baada hajja kubwa na ndogo, nami nilikuwa mmoja katika Swahaba wa Mtume  ﷺ. Kwa hivyo nimekuja kukuuliza je, uliwahi kumsikia akisema chochote katika hilo?” Akajibu: “Ndio. Alikuwa akituamuru tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu siku tatu na masiku yake, isipokuwa tu kutokana na janaba, lakini kutokana na haja kubwa, ndogo na kulala (tusivue).” Nikamuuliza: “Je, ulimsikia akisema chochote juu ya mapenzi?” Akajibu: “Ndio. Tulikuwa na Mtume wa Mwenyez i Mungu ﷺ safarini, tulipokuwa tupo kwake, kwa ghafla akaitwa na Bedui kwa sauti kubwa: “Ee Muhammad!” Mutme  wa Mwenyezi Mungu  akamuitikia kwa sauti kama yake: [Njoo.] Nikamwambia (Bedui): “uko na nini, teremsha sauti yako kwani upo mbele ya Mtume wa Mwneyzi Mungu na umekatazwa jambo hili!” Akasema: “Naapa kwa jina la Mwenyzi Mungu siteremshi!”  Yule Bedui akasema: “Unaonaje kuhusu mtu anapenda watu na bado hajakutana nao?”  Mtume wa Mwenyezi Mungu  akamwambia: [Mtu atakuwa pamoja na ampendae siku ya Qiyama] Basi akaendelea kutuzungumzia mpaka akautaja mlango upande wa magharibi mwendo wa upana wake au atasafiri mpandaji kwa upana huu miaka arobaini au sabini. Akasema Sufyaan mmoja wa wapokezi:  “Upande wa Shamu. Allaah Aliuumba tokea siku Aliyoumba mbingu na ardhi hali ya kuwa umefunguliwa kwa ajili ya Tawba, haufungwi mpaka jua lichomoze upande huo.”    [Imepokewa na At-Tirmidhiy na wengineo, na akasema: Hadiyth hii ni Hasan Sahihi]


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6572807
TodayToday874
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 29

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68286382749378692651121747477378
title_6828638274a4220362196191747477378
title_6828638274b426343787961747477378

NISHATI ZA OFISI

title_6828638274dff6971915361747477378
title_6828638274f014896166871747477378
title_6828638274ffe17821415011747477378 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 12 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com