Menu

BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


قال العلماء: التوبة واجبة مِنْ كل ذنب. فإن كانت المعصية بين العبد وبين اللَّه تعالى لا تتعلق بحق آدمي فلها ثلاثة شروط

أحدها:  أن يقلع عَنْ المعصية

والثاني:  أن يندم عَلَى فعلها

والثالث:  أن يعزم أن لا يعود إليها أبدا؛

فإن فقد أحد الثلاثة لم تصح توبته

وإن كانت المعصية تتعلق بآدمي فشروطها أربعة: هذه الثلاثة وأن يبرأ مِنْ حق صاحبها. فأن كانت مالا أو نحوه رده إليه، وإن كان حد قذف ونحوه مكنه مِنْه أو طلب عفوه، وإن كانت غيبة استحله مِنْها. ويجب أن يتوب مِنْ جميع الذنوب، فإن تاب مِنْ بعضها صحت توبته عند أهل الحق مِنْ ذلك الذنب وبقى عليه الباقي.

وقد تظاهرت دلائل الكتاب والسنة وإجماع الأمة عَلَى وجوب التوبة


Wanachuoni  wamesema: ni wajibu kutubia kwa kila dhambi anayoitenda mtu. na Madhambi yanapokuwa ni baina ya Mwenyezi Mungu ﷻ na mja wake yasiyofungamana na haki ya mwana Aadam, yana shuruti tatu:

1- Ajingoe na ile Dhambi 

2- Ajute juu ya kutenda ile Dhambi 

3- Aazimie kutoyarudia tena kabisa.

Moja katika shuruti hizo ikikosekana, basi Tawba yake haitosihi.

Na Madhambi yanapofungamana na haki ya mwanadamu, basi Masharti ya Tawba huwa ni nne: ni hizo tatu zilizotangulia

4- Na ya Nne ni: aregeshe haki ya mwenyewe; ikiwa ni mali na mfano wake amrejeshee, ikiwa ni haddi (adhabu) ya kutukana au mfano wake, atammakinisha au amuombe msamaha. Na ikiwa ni kusengenya basi atamuomba amhalalishie.

Na niwajibu mtu kutubia juu dhambi zote. na Akitubia baadhi yake, Tawba yake itasihi kutokana na dhambi ile kwa watu wa haki, na atabakiwa na dhambi nyinginezo.

Na zimekuja Dalili nyingi katika Qur'ani, na Sunna na ijmaa’ ya ummah juu ya uwajibu wa kutubia.

Amesema Mwenyezi mungu ﷻ: 

 

{وتوبوا إِلَى اللَّه جميعا أيها المؤمنون لعلكم تفلحون}

 

[Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.]    [An Nuur:32]

Na Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

 

{استغفروا ربكم ثم توبوا إليه}

 

[Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake]    [Huud:3]

Na Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

 

{يا أيها الذين آمنوا توبوا إِلَى اللَّه توبة نصوحا}

 

[Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli!]    [Attahrim:8]


شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

8355446
TodayToday562
Highest 09-30-2026 : 21356
US
Guests 128

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6ac8e0f694e847033428401791549686
title_6ac8e0f694ee77807602211791549686
title_6ac8e0f694f3614502466731791549686

NISHATI ZA OFISI

title_6ac8e0f69573b17936425741791549686
title_6ac8e0f69579b10508677781791549686
title_6ac8e0f6957f93622754221791549686 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

Go to top
UongofuUongofu.com