Menu

الحديث التاسع عشر


Annawawiy1


” احفظ الله يحفظك”

عن أبي العَبَّاس عَبْدِ اللهِ بنِ عَبَّاسٍ رَضي اللهُ عنهما قال: كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: [ يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ

رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ

وَفِي رِوَايَةِ غَيْرِ التِّرْمِذِيِّ

 احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ أَمَامَكَ تَعَرَّفْ إِلى اللهِ فِي الرَّخَاءِ يَعْرِفْكَ فِي الشِّدَّةِ واعْلَمْ أَنَ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ وَما أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ وَاعْلَمْ أنَ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ وَ أَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرَاً


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



 HADITHI YA 19


KUAMINI KADARI YA MWENYEZI MUNGU


Kutoka kwa Abul ‘Abbaas Abdullah Ibn ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yao ambaye alisema:

Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume ﷺ akaniambia: [Kijana nitakufundisha maneno  Mhifadhi Mwenyezi Mungu Atakuhifadhi. Muhifadhi Mwenyezi Mungu na utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Mwenyezi Mungu  ukitafuta msaada tafuta kwa Mwenyezi Mungu. na ujue kuwa ikiwa taifa zima litaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile alichokwishakuandikia Allaah aliye tukuka  na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hotodhurika ila tu kwa kile Allaah aliyetukuka alichokwishakuandikia (kuwa kitakudhuru) . Kwani Kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na sahifa zimeshakauka (Hakuna kupangwa tena wala kupanguliwa).]

[Imepokelewa na At-Tirmidhi akasema kuwa ni hadithi Hasan Sahihi.]

Na kwa mapokezi mengine yasiyokuwa ya At-Tirmidhi inasema:

[Muhifadhi Mwenyezi Mungu  utakuta katangulia mbele yako (kwa ulinzi Wake, himaya na msaada Wake). Mjue Mola wako katika neema (muombe, mche, mtii) Atakujua katika shida (unapokuwa katika dhiki Naye Atakusaidia). Jua kuwa yaliyokukosa hayakuwa yakupate na yaliokupata hayakuwa yakukose. Jua kuwa ushindi uko pamoja na subira, na faraja iko pamoja na dhiki, na raha iko pamoja na shida (haviachani).]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6511896
TodayToday754
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 35

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_67866209189db10119957901736860169
title_6786620918ac18771871801736860169
title_6786620918bac14039789301736860169

NISHATI ZA OFISI

title_678662091a18112200522211736860169
title_678662091a25a15556222381736860169
title_678662091a3361490968971736860169 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com