ANACHOSEMA NA KUFANYA ANAPOSIKIA MAUMIVU
Weka mkono wako juu ya sehemu inayokuuma na kisha useme :
[بِسْمِ اللهِ]
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu] (mara tatu)
Kisha usema mara saba:
[أَعُوذُ باللهِ وَقُدْرَتِهِ مَنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ]
[Najilinda kwa Mwenyezi Mungu na kwa uwezo wake kutokana na shari ya ninachokisikia na ninachokiogopa.] [Imeokewa na Muslim.]
ANACHOSEMA NA KUFANYA ANAPOSIKIA MAUMIVU
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.