ANAPORUSHA KILA KIJIWE KATIKA JAMARAH (NGUZO)
Alikuwa Mtume ﷺ kila anaporusha kijiwe katika Jamarah (nguzo) tatu akisema
[أَللّهُ أَكْبَرُ]
[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa]
….. anapomaliza kurusha vijiwe saba katika Jamarah (nguzo) ya kwanza, alikuwa anasogea mbele kidogo, anasimama kuelekea Qibla hali yakuwa ameiinuwa mikono yake, kisha anaanza kumuomba Mwenyezi Mungu. Alikuwa akifanya hivi katika Jamaaraha ya kwanza na ya pili pekee, ama ya tatu alikuwa hasimami bali akimaliza anaondoka. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.