DUA YA KUJILINDA NA DAJJAL
[ من حفظ عشر آيات من أول سورة الكهف عصم من الدجال ]
مسلم 1/555
Amesema Mtume ﷺ:
[Yoyote anaehifadhi kwa moyo aya kumi za mwanzo wa Suratul-Kahf atakuwa na kinga ya kujiepusha na Dajjal.] [Imepokewa na Muslim.]
Pia ni katika Sunnah kujilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na fitna ya Dajjal baada ya tashahhud ya mwisho katika kila swala.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.