KINGA YA MUISLAMU
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ anapoingia kumzuru mgonjwa akimwambia
[ لا بأس طهور إن شاء الله ]
[Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa (na madhambi) anapopenda Mwenyezi Mungu. ] [Imepokewa na Bukhari.]
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: Hapana mja yeyote muislamu anaemtembelea mjongwa ambae wakati wake wa kufa bado haujafika na akamuombea mara saba
[ أسأل الله العظيم رب العرش العظيم أن يشفيك ]
[Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Arshi tukufu (akuponyeshe)]
Isipokuwa Mwenyezi Mungu humponyesha mgonjwa huyo. [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Abuu Daud.]
DUA YA KUMTEMBELEA MGONJWA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.