KINGA YA MUISLAMU
اللهم باعد بيني وبين خطاياي كما باعدت بين المشرق والمغرب ، اللهم نقني من خطاياي كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس اللهم اغسلني من خطاياي بالماء والثلج والبرد البخاري 1/ 181 ومسلم 1/ 419
[Ewe Mwenyezi Mungu niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi, Ewe Mwenyezi Mungu nitakase na madhambi yangu kama vile inavyoitakaswa nguo nyeupe na uchafu, Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
[ سبحانك اللهم وبحمد ك وتبارك اسمك وتعالى جدك، ولا أ له غيرك]
أخرجه أصحاب السنن الأربعة وانظر صحيح الترمذي 1/77 وصحيح ابن ماجه 1/ 135
[Kutakasika ni Kwako ewe Mwenyezi Mungu , na sifa njema zote ni zako, na limetukuka jina lako, na utukufu niwako, na hapana apasae kuabudiwa kwahaki, asie kuwa wewe.] [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Tirmidhiy na Al-Nasai na Ibnu Maajah.]
وجهت وجهي للذي فطر السموات والأرض حنيفاً وما أنا من المشركين ،إن صلاتي ونُسُكي ومحياي ومماتي لله رب العالمين ، لا شريك له وبذلك أمرت وأنا من المسلمين اللهم أنت الملك لا إله إلا أنت ، أنت ربي وأنا عبدك ، ظلمت نفسي ، واعترفت بذنبي ، فاغفر لي ذنوبي جميعاً ، إنه لا يغفر الذنوب إلا أنت ، واهدني لأحسن الأخلاق، لا يهدي لأحسنها إلا أنت ، واصرف عني سيئها لا يصرف عني سيئها إلا أنت لبيك وسعديك والخير كله بيديك ، والشر ليس إليك ، أنا بك وإليك ، تباركت وتعاليت أستغفرك وأتوب إليك رواه مسلم1/ 534
Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambae ameumba mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika swala yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe vyote, hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa, nami ni katika waislamu. Ewe Mwenyezi Mungu , Wewe ndie mfalme, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, Wewe ndie Bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja) wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamehe madhambi yangu yote, hakika hasamehe madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia njema (nzuri), kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wakuniepusha na tabia mbaya ila Wewe. Naitikia mwito Wako, na ninafuraha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi KWako, umetakasika, na umetukuka, nakutaka msamaha na ninarejea Kwako (kwa kutubia)] [Imepokewa na Muslim.]
اللهم رب جبرائيل وميكائيل وإسرافيل ، فاطر السموات والأرض ، عالم الغيب والشهادة ، أنت تحكم بين عبادك فيما كانوا فيه يختلفون اهدني لما اختلف فيه من الحق بإذنك إنك تهدي من تشاء إلى صراط مستقيم رواه مسلم1/ 534
[Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa Jibiriil na Mikaail na Israafil, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliojificha na yaliowazi, Wewe unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliotafautiana kwa ruhusu Yako. Hakika Wewe unamuongoza umtakae kwenye njia ilionyoka.] [Imepokewa na Muslim.]
الله اكبر كبيرا، الله اكبر كبيرا، الله اكبر كبيرا، والحمد لله كثيرا، والحمد لله كثيرا، والحمد لله كثيرا، وسبحان الله بكرةً وأصيلا ـ ثلاثا ـ " أعوذ بالله من الشيطان الرجيم : من نفخه، ونفثه ، و همزه. أخرجه أبو داود 1/ 203 وابن ماجه 1/ 265 وأحمد 4/85 وأخرجه مسلم عن ابن عمر رضي الله عنهما بنحوه وفيه قصة 1/ 420
[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu , kwa wingi na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni” (Utasema haya mara tatu)Najilindia na Mwenyezi Mungu kutokana na shetani, na kupulizia kwake, na kutabana kwake na kutia kwake wasiwasi katika nyoyo za binaadamu.] [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah na Ahmad na Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Ibnu Umar radhi za Allah ziwe juu kama hivi.]
كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا قام من الليل يتهجد قال: " اللهم لك الحمد أنت نور السموات والأرض ومن فيهن ، ولك الحمد أنت قيمُ السموات والأرض ومن فيهن [ ولك الحمد أنت رب السموات والأرض ومن فيهن ] [ ولك الحمد لك ملك السموات والأرض ومن فيهن ] [ ولك الحمد أنت ملك السموات والأرض] [ ولك الحمد] أنت الحق ، ووعدك الحق ، وقولك الحق ،ولقاؤك الحق ، والجنة حق ، والنار حق ، والنبيّون حق ومحمد صلى الله عليه وسلم حق والساعة حق ] [اللهم لك أسلمت ، وعليك توكلت ، وبك آمنت ، وإليك أنبت ، وبك خاصمت ، وإليك حاكمت ، فاغفر لي ما قدمت وما أخرت ، وأسررت، وما أعلنت ] [ أنت المقدم ،وأنت المؤخر لا إله إلا أنت ] [أنت إلهي لا إله إلا أنت البخاري مع الفتح 3/3 و11/116 و 13/ 371 423، 465 ومسلم مختصراً بنحوه 1/ 532
Mtume ﷺ alikuwa akiamka usiku ili kufanya ibada anasema :
[Ewe Mwenyezi Mungu ni Zako sifa njema, Wewe ndie nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na nizako sifa njema. Wewe ndie sababu ya kusimama kwa mbingu na archi na vilivyomo ndani yake, na nizako sifa njema, Wewe ndie Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na nizako sifa njema, Wewe ndiye Mfalme wa mbingu na ardhi, na nizako sifa njema, Wewe ni Haki (kweli) na ahadi yako ni yakweli, na neno lako ni lakweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na pepo ni kweli, na moto ni kweli, na Mitume ni kweli, na Muhammad ﷺ ni kweli, na Qiyama ni kweli, Ewe Mwenyezi Mungu , Kwako nimejisalimisha, na kwako nimetegemea, nawewe nimekuamini, na Kwako nimerejea na kwa ajili yako nimeteta, na kwako nimehukumu, kwa hivyo nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza; Wewe ndiye mwenye kuchelewesha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe; Wewe ndie Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.