Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitab altawheed


باب الشفاعة
{وقول الله عز وجل: {وَأَنْذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْ يُحْشَرُوا إِلَى رَبِّهِمْ لَيْسَ لَهُمْ مِنْ دُونِهِ وَلِيٌّ وَلا شَفِيعٌ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

{وقوله: {قُلْ لِلَّهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعاً

:وَقَوْلِهِ

{مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ}

:وَقَوْلِهِ

{وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ}

:وَقَوْلِهِ

{قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ}

قَالَ أَبُو الْعَبَّاسِ، نَفَى اَللَّهُ عَمَّا سِوَاهُ كُلَّ مَا يَتَعَلَّقُ بِهِ الْمُشْرِكُونَ، فَنَفَى أَنْ يَكُونَ لِغَيْرِهِ مُلْكٌ أَوْ قِسْطٌ مِنْهُ أَوْ يَكُونَ عَوْنًا لِلَّهِ وَلَمْ يَبْقَ إِلاَّ اَلشَّفَاعَةُ، فَبَيَّنَ أَنَّهَا لاَ تَنْفَعُ إِلاَّ لِمَنْ أَذِنَ لَهُ اَلرَّبُّ، كَمَا قَالَ: {وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ

فَهَذِهِ اَلشَّفَاعَةُ اَلَّتِي يَظُنُّهَا الْمُشْرِكُونَ هِيَ مُنْتَفِيَةٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، كَمَا نَفَاهَا الْقُرْآنُ، وَأَخْبَرَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ يَأْتِي فَيَسْجُدُ لِرَبِّهِ وَيَحْمَدُهُ لاَ يَبْدَأُ بِالشَّفَاعَةِ أَوَّلاً - ثُمَّ يُقَالُ لَهُ :اِرْفَعْ رَأْسَكَ وَقُلْ يُسْمَعْ وَسَلْ تُعْطَ وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ

وَقَالَ لَهُ أَبُو هُرَيْرَةَ رضي اَللَّهُ عَنْهُ: مَنْ أَسْعَدُ اَلنَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ؟ قَالَ: [مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ

[فَتِلْكَ اَلشَّفَاعَةُ لأَهْلِ الإِخْلاصِ بِإِذْنِ اَللَّهِ، وَلا تَكُونُ لِمَنْ أَشْرَكَ بِاَللَّهِ

وَحَقِيقَتُهُ أَنَّ اَللَّهَ سُبْحَانَهُ هُوَ اَلَّذِي يَتَفَضَّلُ عَلَى أَهْلِ الإِخْلاصِ، فَيَغْفِرُ لَهُمْ بِوَاسِطَةِ دُعَاءِ مَنْ أَذِنَ لَهُ أَنْ يَشْفَعَ، لِيُكْرِمَهُ وَيَنَالَ الْمَقَامَ الْمَحْمُودَ

فَالشَّفَاعَةُ اَلَّتِي نَفَاهَا الْقُرْآنُ مَا كَانَ فِيهَا شِرْكٌ، وَلِهَذَا أَثْبَتَ اَلشَّفَاعَةَ بِإِذْنِهِ فِي مَوَاضِعَ وَقَدْ بَيَّنَ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهَا لاَ تَكُونُ إِلاَّ لأَهْلِ الإِخْلاصِ وَالتَّوْحِيدِ. اِنْتَهَى كَلامُهُ


MLANGO WA 16 UOMBEZI


Ni kauli ya Mwenyezi Mungu :

[Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu.]  [Al-An’aam: 51]

Na kauli Yake :

[Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake]   [Az-Zumar: 44]

Na kauli Yake :

[Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake?]  [Al-Baqarah: 255]

Na kauli Yake :

[Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.]  [An-Najm: 26]

Na kauli Yake :

[Sema: “Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini]  [Sabaa: 22]

Amesema Abuu Al-‘Abbaas (Ibnu Taymiyah):  “Mwenyezi Mungu Amekanusha kila kisichokuwa Yeye ambacho washirikina wanawanyenyekea. Akakanusha kuwa hakuna isipokuwa yeye Mwenyezi Mungu Mwenye milki na uwezo. Hakuna mwenye kusaidia ila Yeye. Kinachobaki ni shafaa’ah. Akabainisha kwamba hautomfaa yeyote isipokuwa ambaye amepewa idhini ya Mwenyezi Mungu kama Anavyosema: [Wala hawamwombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.]    [Al-Anbiyaa: 28]

Kwa sababu hiyo Uombezi wanayoiamini washirikna itakanushwa Siku ya Qiyama kama ilivyokanushwa na Qur'ani na Mtume alitolea habari kwamba: Atafika kisha atamsujudia Mola wake atamhimidi, na hataombea kwanza kwa. Kisha itasemwa: “Inua kichwa chako! Sema utasikilizwa! Omba utapewa! Omba shafaa’ah utaruhusiwa kuombeza] [Al-Bukhaariy na Muslim]

Abuu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu yake) alimuuliza Mtume : “Nani atakayefanikiwa zaidi na uombezi wako? Akajibu: [Atakayesema Laa ilaaha illa-Allaah, (Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa na niyyah safi moyoni mwake]   [Imepokewa na Bukhari]

Basi hiyo ndio uombezi kwa watu wenye ikhlas kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wala haitokuwa kwa anayemshirikisha Mwenyezi Mungu.

Na uhakika wake (shafaa’ah hiyo) ni kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye Anayewafanyia ihsaan watu wenye ikhlas (katika ‘ibada zao). Atawasamehe kwa kupitia  du’a au shafaa kwa aliepewa idhini ya kuombea ili Amkirimu na aweze kufikia cheo cha Al-Maqaam Al-Mahmud.

na uombezi (shafaa’a) inayokanushwa na Qur'ni ni iliyo na shirki, na ndio maana shafaa’ah imethibiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu sehemu nyingi na Mtume  amebainisha kwamba shafaa’a haitokuwa isipokuwa kwa watu wa Tawhiyd na ikhlas [katika Dini yao]” -  Mwisho wa maneno ya Ibn Taymiyyah.

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Tafsiri ya Aya zilizotajwa.

2. Maelezo ya aina ya shafaa’ah iliyokanushwa.

3. Maelezo ya aina ya shafaa iliyothibiti.

4. Kutajwa uombezi mkuu wa Mtume  na kuhusu Al-Maqaam Al-Mahmud.

5. Atakalofanya Mtume , na kwamba hatoanza na shafaa, bali atasujudu, halafu atakapopewa idhini ndipo atakapoinuka kuombea shafaa.

6. Nani atakayefaidika kupata hadhi hiyo ya shafaa’ah ya Mtume ﷺ ?

7. Shafaa haitokuwa kwa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu ﷻ.

8. Kubainisha ukweli wa shafaa.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487138
TodayToday244
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 35

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e572c3975b21002450911735284524
title_676e572c3984618995593421735284524
title_676e572c399295117024941735284524

NISHATI ZA OFISI

title_676e572c3b06411153331631735284524
title_676e572c3b1584312109401735284524
title_676e572c3b23c15740847021735284524 Add content here

HUDUMA MPYA

: 7 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com