Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitab altawheed


باب (15) قول الله تعالى: {حَتَّى إِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ}  سبأ:23

في الصحيح عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: "إذا قضى الله الأمر في السماء ضربت الملائكة بأجنحتها خضعانا لقوله، كأنه سلسلة على صفوان ينفذهم ذلك {حَتَّى إِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ}  فيسمعها مسترق السمع - ومسترق السمع هكذا بعضه فوق بعض - وصفه سفيان بكفه فحرفها وبدد بين أصابعه - فيسمع الكلمة فيلقيها إلى من تحته، ثم يلقيها الآخر إلى من تحته، حتى يلقيها على لسان الساحر أو الكاهن. فربما أدركه الشهاب قبل أن يلقيها، وربما ألقاها قبل أن يدركه، فيكذب معها مائة كذبة. فيقال: أليس قد قال لنا يوم كذا وكذا كذا وكذا؟ فيصدق بتلك الكلمة التي سمعت من السماء
وعن النواس بن سمعان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: "إذا أراد الله تعالى أن يوحي بالأمر تكلم بالوحي أخذت السموات منه رجفة - أو قال رعدة - شديدة خوفا من الله ؛ فإذا سمع ذلك أهل السموات صعقوا، وخروا لله سجدا. فيكون أول من يرفع رأسه جبريل، فيكلمه الله من وحيه بما أراد. ثم يمر جبريل على الملائكة، كلما مر بسماء سأله ملائكتها: ماذا قال ربنا يا جبريل؟ فيقول جبريل قال الحق وهو العلي الكبير فيقولون كلهم مثل ما قال جبريل فينتهي جبريل بالوحي إلى حيث أمره الله"
:فيه مسائل
الأولي: تفسير الآية
الثانية: ما فيها من الحجة على إبطال الشرك، خصوصا ما تعلق على الصالحين، وهي الآية التي قيل: إنها تقطع عروق شجرة الشرك من القلب
الثالثة: تفسير قوله: {قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ} 1
الرابعة: سبب سؤالهم عن ذلك
"الخامسة: أن جبرائيل يجيبهم بعد ذلك بقوله: " قال كذا وكذا
السادسة: ذكر أن أول من يرفع رأسه جبرائيل
السابعة: أنه يقول لأهل السموات كلهم، لأنهم يسألونه
الثامنة: أن الغشي يعم أهل السموات كلهم
التاسعة: ارتجاف السموات بكلام الله
العاشرة: أن جبرائيل هو الذي ينتهي بالوحي إلى حيث أمره الله
الحادية عشرة: ذكر استراق الشياطين.الثانية عشرة: صفة ركوب بعضهم بعضا
الثالثة عشرة: إرسال الشهاب
الرابعة عشرة: أنه تارة يدركه الشهاب قبل أن يلقيها، وتارة يلقيها في أذن وليه من الإنس قبل أن يدركه
الخامسة عشرة: كون الكاهن يصدق بعض الأحيان
السادسة عشرة: كونه يكذب معها مائة كذبة
السابعة عشرة: أنه لم يصدق كذبه إلا بتلك الكلمة التي سمعت من السماء
الثامنة عشرة: قبول النفوس للباطل، كيف يتعلقون بواحدة، ولا يعتبرون بمائة 2؟
التاسعة عشرة: كونهم يتلقى بعضهم من بعض تلك الكلمة، ويحفظونها ويستدلون بها
العشرون: إثبات الصفات، خلافا للأشعرية المعطلة
الحادية والعشرون: أن تلك الرجفة والغشي خوف من الله
الثانية والعشرون: أنهم يخرون لله سجدا


MLANGO WA 15 NENO LA MWENYEZI MUNGU: {HATA ITAPO ONDOLEWA KHOFU KWENYE NYOYO ZAO WATASEMA: MOLA WENU MLEZI KASEMA NINI? WATASEMA: YALIYO KWELI ! NA YEYE NDIYE ALIYE JUU, MKUBWA }


Na katika Swahih (Al Bukhari) Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amepokea kutoka kwa Mtume amesema: [Mwenyezi Mungu Anapohukumu jambo mbinguni, Malaika hupiga mbawa zao kwa kuinyenyekea kauli ya wahyi wa Mwenyezi Mungu, kwa vile Malaika husikia kama kwamba ni sauti za minyororo ya chuma inyoburutwa katika juu ya jiwe gumu. Huwakumba na kuwakhofisha hadi wazimie,hubaki katika hali hiyo mpaka Jibrili anawajia na kumuliza Jibril huwambia kuwa hilo ni Neno la Haki, [Hata itapo ondolewa khofu kwenye nyoyo zao watasema: Mola wenu Mlezi kasema nini? Watasema: Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa.] Watasikia amri hii wadukizi wa siri [wezi wa Maneno nao ni Mashetani].  Na wasikivu wa siri hao wako kama hivi; wanarundikana mmoja juu ya wengine)): Sufyaan alionyesha kwa kuunyanyua mkono wake na kutawanya vidole. husikia neno ambalo hulipeleka kwa aliyechini yake, na wa pili hulipeleka kwa aliye chini yake, hubadilishabadilisha katika kupokeana kauli hiyo mpaka wa mwisho wao ambaye hulipeleka kwa mchawi au kuhani. Mara nyingine kimondo humpiga Shetani kabla ya kuwahi kuipeleka na mara nyingine huwahi kuipeleka kabla kimondo hakijampiga. Hapo mchawi huongezea uongo wake mara mia kuhusu neno hilo. Watu [huku ulimwenguni] husema: Je hatukujulisha kadha na kadhaa siku kadhaa na kadhaa. Hivyo mchawi huaminiwa kwa kuwa kasema ukweli kutokana na kauli iliyosikika mbinguni   

Kutoka kwa An-Nawaas bin Sam’aan (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: [Mwenyezi Mungu Anapotaka kuleta Wahyi wa jambo, Hutamka na mbingu hutetemeka kwa nguvu)) Au kasema: ((Radi ya nguvu kwa kumkhofu Mwenyezi Mungu ﷻ . Wanapoyasikia Malaika wa mbinguni, huzimia au huporomoka na kusujudu. Wa kwanza anayeinua kichwa chake huwa ni Jibriyl. Kisha Mwenyezi Mungu Humsemesha kumpa Wahyi kwa analolitaka. Kisha Jibriyl huwapitia Malaika. Kila anapopita kwenye mbingu Malaika wake humuuliza: Amesema nini Mola wetu Ewe Jibriyl?  Jibril Husema: Amesema Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa. Wote husema kama alivyosema Jibril. Jibril anaishia kuufikisha Wahyi alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu ]   [Ibn Khuzaymah fiy At-Tawhiyd (206)]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Tafsiri ya Ayah (katika Sura Sabaa:23)

2. Yaliyomo humo miongoni mwa hoja kuu ya kubatilisha shirki hususani kwa wenye kutegemea waja wema (kwa kuwaomba). na ndio Aya hii iliyosemwa kuwa ndiyo Aya inayokata mizizi ya shirki.

3. Tafsiri ya neno lake Mwenyezi Mungu: [Watasema: Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa.]

4. Sababu ya (Malaika) Kuuliza kwao wao swali hilo 

5. Kuwa Jibril huwajibu Baada ya hapo, swali lao kwa kusema, “Amesema kadhaa wa kadhaa.”

6. Kutajwa kuwa wa kwanza atakayeinua kichwa chake ni Jibril.(Alayhi salaam)

7. Jibril huwaambia Malaika wote walioko mbinguni kwa sababu wamemuuliza.

8. Kuzimia (kwa Athari ya tetemeko) linawaenea wakazi wote wa mbinguni.

9. Kutetemka mbingu kutokana na Maneo ya Mwenyezi Mungu .

10. Kwamba Jibriyl ndiye anayepeleka Wahyi mahali Anapomwamuru Mwenyezi Mungu .

11. Kutajwa udukuzi wa shetani (kusikiliza siri).

12. Kuelezea sifa ya Kupandiana kwa majini mmoja juu ya mwingine.

13. Kufyatuliwa vimondo (vya moto.)

14. Wakati mwingine vimondo vinamkuta kabla hawajafikisha khabari, na wakati mwingine kuifikisha khabari katika sikio la rafiki yake, binadamu kabla kimondo kumfikia.

15. Huenda Wakati mwingine kuhani (mchawi) akasema ukweli.

16. Pamoja na urongo wake huongezea uongo mara mia.

17. (Makuhani) hawasadikiwi urongo wao ila kwa lile neno walilosikia kutoka mbinguni.

18. Kuonyesha vile Nafsi zinavyo kubali Batili Vipi wanategemea ukweli mmoja na kutokuzingatia mara 99 ya uongo wake?

19. Jinsi (Mashetani) wanavyopashana maneno na wanayahifadhi na kuyatumia kama dalili (ya uongo mwingine).

20. Kuthibitisha Sifa za Mwenyezi Mungu  kinyume na Ash‘ariyyah wenye kuziawili sifa zake.

21. Kwamba Ngurumo na tetemeko la mbingu ni kwa ajili ya kumkhofu Mwenyezi Mungu  .

22. Kwamba Malaika wanaporomoka chini kumsujudia Mwenyezi Mungu (baada ya kusikia maneno Yake.)


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487243
TodayToday349
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 51

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5ab82a64f10914339581735285432
title_676e5ab82a74a19795092731735285432
title_676e5ab82a8473187796501735285432

NISHATI ZA OFISI

title_676e5ab82bff616632213481735285432
title_676e5ab82c0eb18362659641735285432
title_676e5ab82c1de5163565611735285432 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com