Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitab altawheed


باب من الشرك: لبس الحلقة والخيط ونحوهما لرفع البلاء أو دفعه

قول الله تعالى: {قُلْ أَفَرَأَيْتُمْ مَا تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ قُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ
عن عمران بن حصين رضي الله عنه: [أن النبي صلى الله عليه وسلم رأى رجلا في يده حلقة من صفر فقال: ما هذه؟ قال من الواهنة. فقال: انزعها، فإنها لا تزيدك إلا وهنا؛ فإنك لو مت وهي عليك ما أفلحت أبدا] .   رواه أحمد بسند لا بأس به
وله عن عقبة بن عامر مرفوعا: [ من تعلق تميمة فلا أتم الله له، ومن تعلق ودعة فلا ودع الله له ]     رواه احمد

وفي رواية: [ من تعلق تميمة فقد أشرك ]      رواه أحمد
{ولابن أبي حاتم عن حذيفة "أنه رأى رجلا في يده خيط من الحمى، فقطعه وتلا قوله: {وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُمْ بِاللَّهِ إِلاَّ وَهُمْ مُشْرِكُونَ

فيه مسائل
الأولي: التغليظ في لبس الحلقة والخيط ونحوهما لمثل ذلك
الثانية: أن الصحابي لو مات وهي عليه ما أفلح. فيه شاهد لكلام الصحابة أن الشرك الأصغر أكبر من الكبائر
الثالثة: أنه لم يعذر بالجهالة
الرابعة: أنها لا تنفع في العاجلة، بل تضر لقوله: "لا تزيدك إلا وهنا" 1
الخامسة: الإنكار بالتغليظ على من فعل مثل ذلك
السادسة: التصريح بأن من تعلق شيئا وُكل إليه
السابعة: التصريح بأن من تعلق تميمة فقد أشرك
الثامنة: أن تعليق الخيط من الحمى من ذلك
التاسعة: تلاوة حذيفة الآية دليل على أن الصحابة يستدلون بالآيات التي في الشرك الأكبر على الأصغر، كما ذكر ابن عباس في آية البقرة
العاشرة: أن تعليق الودع عن العين من ذلك
الحادية عشرة: الدعاء على من تعلق تميمة أن الله لا يتم له، ومن تعلق ودعة فلا ودع الله له، أي ترك الله له


MLANGO WA 07 NI SHIRK KUVAA KIKUKU CHA CHUMA NA UZI NA VITU KAMA HIVYO KWA AJILI YA KUONDOSHA AU KUZUIA BALAA


Na neno lake Mwenyezi Mungu :

[Sema: Je! Mnawaonaje wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemee wanao tegemea.]    [Azzumar: 38]

Na kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn  (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume  alimwona mtu amevaa kikuku cha chuma mkononi mwake, akamuuliza: [Nini hiki?] Akajibu: “Kuzuia udhaifu wa uzee.” Akasema: [Ivue, kwani haizidishi ila udhaifu. Na pindi ukifa ukiwa nacho, hutofaulu kamwe]   [Imepokelewa na Ahmad katika Musnad kwa isnaad nzuri]

Na pia Ahmad amepokea kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhi za Allah ziwe juu yake) Hadith Marfuw (kutoka kwa Mtume )  Amesema: [Atakayetundika hirizi hatopata kuona haja yake kutimizwa na Mwenyezi Mungu. Na atakayeitundika kombe la pwani hatopata amani na utulivu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.]   [Imepokewa naAhmad katik Musnad]

Na katika riwaya nyingine: [Atakayetundika hirizi ameshirikisha]   [Imepokewa na Ahmad]

Na amepokea Ibn Haatim kutoka kwa Hudhayfa (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa alimuona mtu amefunga uzi kwenye mkono wake kwa ajili ya kukinga homa akaukata kisha akasoma kauli yake Mwenyezi Mungu [Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina.]    [Yusuf:106]   

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1- Haramisho la kuvaa vikuku vya chuma nyuzi na mfano wake kwa ajili ya kinga

2- Ikiwa Swahaba  lau atakufa hali amevaa (Hirizi au uzi) hatofaulu. Huu ni ushahidi ya kauli ya Maswahaba kuwa shirki ndogo ni mbaya zaidi kuliko Madhambi makubwa.

3- Kwamba mtu hatopewa Udhuru kwa sababu ya Ujinga.

4- Kuvaa vitu kama hivyo, havitomnufaisha mtu hapa duniani bali vitadhuru kama alivyosema Mtume : [haizidishi ila udhaifu].

5- Kemeo kali kwa mwenye kufanya jambo kama hili.(La kuvaa hirizi na mfano wake)

6- Kubainsha wazi kuwa mtu anapovaa vitu hivi anakuwa ameachwa alindwe na hivyo vitu (badala ya kulindwa na Mwenyezi Mungu.)

7- Maelezo ya wazi kuwa mwenye kuvaa hirizi amefanya shirki.

8- Kujifunga Uzi kwa ajili ya homa ni sawa na hayo ya kuwa ni shirki.

9- Kusoma Hudhafa (Radhi za Alla ziwe juu yake ) Aya ya Qur'ani ni dalili ya wazi kwamba Maswahaba walikuwa wakitolea dalili Aya inayohusu shirki kubwa kwa ajili ya kukanusha shirki ndogo, kama alivyofanya Ibn ‘Abbaas (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuisoma Aya ya Suratul Baqara.

10- Kwamba Kuvaa hirizi kwa ajili ya kujilinda na jicho baya ni katika hayo (ya ushirikina)

11- Kumuapiza mwenye kuvaa hirizi, kuwa Mwenyezi Mungu Hatomtimizia maombi yake. Na anayejifunga na kombe (la kiumbe wa baharini), hatokuwa katika amani na utulivu yaani Mwenyezi Mungu atamuacha.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487103
TodayToday209
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 53

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e572c3975b21002450911735284524
title_676e572c3984618995593421735284524
title_676e572c399295117024941735284524

NISHATI ZA OFISI

title_676e572c3b06411153331631735284524
title_676e572c3b1584312109401735284524
title_676e572c3b23c15740847021735284524 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com