KITAAB AT-TAWHIID
باب تفسير التوحيد وشهادة أن لا إله إلا الله
{وقول الله تعالى: {أُولَئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَى رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُوراً
{وقوله: {وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِمَّا تَعْبُدُونَ إِلاَّ الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
{وقوله: {اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَاباً مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ
{وقوله: {وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَاداً يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبّاً لِلَّهِ
وفي الصحيح عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: [من قال لا إله إلا الله وكفر بما يُعبد من دون الله، حرم ماله ودمه، وحسابه على الله] وشرح هذه الترجمة: ما بعدها من الأبواب
:فيه أكبر المسائل وأهمها
، وهي تفسير التوحيد، وتفسير الشهادة؛ وبينها بأمور واضحة
منها: آية الإسراء بين فيها الرد على المشركين الذين يدعون الصالحين ففيها بيان أن هذا هو الشرك الأكبر
ومنها: آية براءة، بين فيها أن أهل الكتاب اتخذوا أحبارهم ورهبانهم أربابا من دون الله، وبين أنهم لم يؤمروا إلا بأن يعبدوا إلها واحدا، مع أن تفسيرها الذي لا إشكال فيه: طاعة العلماء والعباد في المعصية، لا دعاؤهم إياهم
ومنها: قول الخليل عليه السلام للكفار: {إِنَّنِي بَرَاءٌ مِمَّا تَعْبُدُونَ إِلاَّ الَّذِي فَطَرَنِي} فاستثنى من المعبودين ربه . وذكر سبحانه أن هذه البراءة وهذه الموالاة هي: تفسير شهادة أن لا إله إلا الله؛ فقال: {وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
ومنها: آية البقرة في الكفار الذين قال الله فيهم: {وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ} . ذكر أنهم يحبون أندادهم كحب الله؛ فدل على أنهم يحبون الله حبا عظيما ولم يدخلهم في الإسلام. فكيف بمن أحب الند أكبر من حب الله؟ فكيف بمن لم يحب إلا الند وحده ولم يحب الله؟
[ومنها: قوله صلى الله عليه وسلم: [من قال لا إله إلا الله وكفر بما يُعبد من دون الله حرم ماله ودمه، وحسابه على الله
وهذا من أعظم ما يبين معنى " لا إله إلا الله "، فإنه لم يجعل التلفظ بها عاصما للدم والمال، بل ولا معرفة معناها مع لفظها، بل ولا الإقرار بذلك، بل ولا كونه لا يدعو إلا الله وحده لا شريك له، بل لا يحرم ماله ودمه حتى يضيف إلى ذلك الكفر بما يعبد من دون الله؛ فإن شك أو توقف لم يحرم ماله ودمه
فيالها من مسألة ما أعظمها وأجلها! وياله من بيان ما أوضحه! وحجة ما أقطعها للمنازع
MLANGO WA TAFSIRI YA TAWHIDI NA SHAHADA YA KWAMBA HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAKI ILA MWENYEZI MUNGU
Na neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo.] [Al-Israa: 57]
Na neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu,Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.] [Az-Zukhruf: 26-28]
Na kauli yake:
[Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu] [At-Tawbah (9: 31)]
Na kauli Yake:
[Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti walio dhulumu wakajua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu!] [Al-Baqarah: 165]
Na katika Hadithi sahihi, kwamba Mtume ﷺ amesema: [Mwenye kusema: laa ilaaha illa-Allaah, (Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu) na akakanusha yote yanayoabudiwa asiekuwa Mwenyezi Mungu, basi imeharamishwa mali yake na damu yake na hisabu yake itakuwa kwa Mwenyezi Mungu] [Imepokewa na Muslim na Ahmad]
Na Sherehe ya Mlango huu na Milango inyofuatia.
Na katika Mlango huu umetaja Mas'ala Makumbwa na Masuala Muhimu Yaliyomo ni:
1- Ni tafsiri ya Tawhid (kumpwekesha Mungu) na Tafsiri ya Shahaadah na kubainisha kwake kwa mambo yaliyo wazi.
2- Mojawapo ni Aya ya Suratul-Israa, imebainisha na kuwarudi washirikina ambao wanawaomba watu wema na kubainisha kwamba kufanya hivyo ni shirki kubwa.
3- Pia Aya ya Suratul-Baraa (At-Tawbah) imebainisha wazi kwamba Ahlul-Kitaab [Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu,]. na ikabinisha ya kwamba wao hawakuamrishwa isipokuwa Kumuabudu Mungu mmoja pamoja na kujua kuwa Tafsiri ya Aya haina utata kuwa kuwatii wanachuoni na waja wema katika masia (kuamuru kufanya Masia) wala sio kuwaomba wao.
4- Pia kauli ya Ibrahim (Amani ya Allah iwe juu yake) kwa makafiri,aliposema:
[Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu,Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa].
Ibraahim (عليه السلام) Alipojiweka mbali na Viabudiwa asiekuwa Mwenyezi mungu kisha akathibitisha Ibada kwa Mola wake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja kuwa Kujitenga (Mushrikina) na kuwa karibu na (waumini) hiyo ndio Tafsiri ya Kushuhudia kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki Ila Mungu mmoja tu (Mungu) akasema :[Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.].
5- Aya katika Suratul-Baqarah kuhusu makafiri ambayo Mwenyezi Mungu Anasema:
[Wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni] [Al-Baqarah: 167)]
Aya hii Imetaja kwamba washirikina wanawapenda miungu yao, kama wanavyompenda Mwenyezi Mungu. Na Aya imedulisha kwamba mapenzi yao juu ya Mwenyezi Mungu ni makubwa, lakini hilo halikuwaingiza katika Uislamu. Itakuwaje hali ya wanaowapenda Masanamu zaidi kuliko Mwenyezi Mungu? Itakuwaje hali ya mtu asiependa ila Masanamu tu na hakumpenda Mwenyezi Mungu?
6-Neno lake Mtume ﷺ amesema:
[Mwenye kusema: laa ilaaha illa-Allaah, (Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu) na akakanusha yote yanayoabudiwa asiekuwa Mwenyezi Mungu, basi imeharamishwa mali yake na damu yake na hisabu yake itakuwa kwa Mwenyezi Mungu]
Hii ni kauli nzito kabisa ya kufafanua Maana ya laa ilaaha illa-Allaah. Inadhihirisha kwamba kuitamka tu hailindi damu na mali ya mtu. Wala haitoshelezi kufahamu maana yake au kuikiri, au hata awe hamuombi mwengine isipokuwa Mwenyezi Mungu ﷻ Pekee; bali mali na damu ya mtamkaji haiharamishwi mpaka juu ya hayo iweko nyongeza ya kwamba, akanushe kabisa kila kinachoabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Na akitilia shaka au akiwa anasitasita, basi mali na damu yake haitokuwa ni haramu.
Ni Mas'ala muhimu yalioje! Mas'ala ya uwazi! Na ni bayana wazi ilioje! na hoja wazi yenye kuondosha mzozo.
Today | 426 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.