AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)
الْمَرْتَبَةُ الثَّانِيَةُ: الإِيمَانُ
وَهُوَ:
[بِضْعٌ وَسَبْعُونَ شُعْبَةً، فَأَعْلاهَا قَوْلُ لا إلٰه إِلا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ]
وَأَرْكَانُهُ سِتَّةٌ كما فى الحديث:
أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ] رواه مسلم]
:وَالدَّلِيلُ عَلَى هَذِهِ الأَرْكَانِ السِّتَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى
لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ} البقرة:177}
:ودليل القدر قَوْلُهُ تَعَالَى
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ} القمر:49}
Daraja Ya Pili: Imani
Nayo ni:
[Ina tanzu (matawi) Sabiini na kitu. Ya juu yake ni kauli ya "Laa ilaaha illa-Allaah” [hapana Muabudiwa wa haki ila Mwenyzi Mungu], na ya chini yake kabisa ni kuondosha uchafu njiani.Na kuona hayaa ni utanzu [tawi] katika tanzu za Imani] (1)
Na nguzo zake ni sita kama ilivyo kuja katika Hadithi:
[Ni kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mitume Wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Qadari kheri yake na shari zake]. [Imepokewa na Muslim]
Na dalili ya hizi nguzo sita ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii,] [Al-Baqara:177]
Na dalili ya Al-Qadr (majaaliwa) ni kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.] [Al-Qamar:49]
SHEREHE YA KITABU USUULU THALATHA NA SHEIKH SHADDAD ALI
1) Hii ni Hadithi iliopokewa na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Alke.
Today | 600 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.