Menu

AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)


misingi


الأَصْلُ الثَّانِي: مَعْرِفَةُ دِينِ الإِسْلامِ بِالأَدِلَّةِ

وَهُوَ :الاسْتِسْلامُ للهِ بِالتَّوْحِيدِ، وَالانْقِيَادُ لَهُ بِالطَّاعَةِ، وَالْبَرَاءَةُ مِنَ الشِّرْكِ وَأَهْلِهِ، وَهُوَ ثَلاثُ مَرَاتِبَ: الإسْلامُ، وَالإِيمَانُ، وَالإِحْسَانُ. وَكُلُّ مَرْتَبَةٍ لَهَا أَرْكَانٌ

المرتبة الأولى: الإسلام
:فَأَرْكَانُ الإِسْلامِ خَمْسَةٌ

شَهَادَةُ أَن لا إلٰه إِلا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَإِقَامُ الصَّلاةِ، وَإِيتَاء الزَّكَاةِ، وَصَوْمُ رَمَضَانَ، وَحَجُّ بَيْتِ اللهِ الْحَرَام

:فَدَلِيلُ الشَّهَادَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ} آل عمران:18}

وَمَعْنَاهَا :لا مَعْبُودَ بِحَقٍّ إلا اللهُ، وَحَدُّ النَّفْيِ مِنْ الإِثْبَاتِ ((لَا إِلَـٰهَ)) نَافِيًا جَمِيعَ مَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللهِ ((إلاَّ الله)) مُثْبِتًا الْعِبَادَةَ للهِ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ فِي عِبَادَتِهِ، كَمَا أَنَّهُ لَيْسَ لَهُ شَرِيكٌ فِي مُلْكِهِ

:وَتَفْسِيرُهَا الَّذِي يُوَضِّحُهَا قَوْلُهُ تَعَالَى

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ الزخرف:26-28

:وقَوْلُهُ تَعَالَى

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ آل عمران:64

:وَدِليلُ شَهَادَةِ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ قَوْلُهُ تَعَالَى

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ} التوبة:128}

وَمَعْنَى شَهَادَة أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ الله: طَاعَتُهُ فِيمَا أَمَرَ، وَتَصْدِيقُهُ فِيمَا أَخْبَرَ، واجْتِنَابُ مَا نَهَى عَنْهُ وَزَجَرَ وأَلا يُعْبَدَ اللهُ إِلا بِمَا شَرَعَ

:وَدَلِيلُ الصَّلاةِ، وَالزَّكَاةِ، وَتَفْسِيرُ التَّوْحِيدِ قَوْلُهُ تَعَالَى

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ} البينة:5}
:وَدَلِيلُ الصِّيَامِ قَوْلُهُ تَعَالَى

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ} البقر:183}

:وَدَلِيلُ الْحَجِّ قَوْلُهُ تَعَالَى

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ} آل عمران:97}


Msingi Wa Pili: Kuijua Dini Ya Kiislamu Kwa Dalili

Nayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa Kumpwekesha, na kunyenyekea katika utiifu, na kujiweka mbali na shirki pamoja na watu wake (washirikina), nao (huo Msingi wa pili) umegawanyika katika daraja tatu; Uislamu, Imani, Ihsaan. Na kila daraja ina nguzo.

Daraja Ya Kwanza: Uislamu

Na nguzo za Kiislamu ni Tano:

Kushuhudia kwa kukiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hakuna Mola apasae Kuabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Swala, na kutoa Zaka, na kufunga Mwezi Ramadhwaan, na kuhiji Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu (Alkaaba).

Na dalili ya Shahada ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.] [Al 'Imran:18]

Na maana yake ni: Hakuna Muabudiwa wa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja. na taarifu yake ni kukanyusha katika kuthibisha temko la (Laa ilaaha) ni kukanusha kila kinachoabudiwa asie kuwa Mwenyezi Mungu. na temko (illa-Allaah) ni kuthibitisha kuwa Ibada zote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Pekee. Hana mshirika katika Ibada Zake kama Alivyokuwa hana mshirika katika Ufalme Wake.

Na tafsiri inayobainisha wazi (Shahada), ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu,Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.] [Azzukhruf:26-28]

Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu.] [Suurat Al 'Imran:64]

Na dalili ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu ni neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.] [Tawba:128]

Na Maana ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kumtii kwa yale aliyoyaamrisha, na kumsadikisha katika aliyoyajulisha, na kujiepusha na ambayo ameyakataza na aliyoyatahadharisha, na kwamba Mwenyezi Mungu asiabudiwe isipokuwa kwa kufuata yale yaliyowekewa Sheria.

Na dalili ya Swala na Zaka na tafsiri ya At-Tawhid (kumpekesha Mungu) ni neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.] [Al-Bayyinah:5]

Na dalili ya Kufunga (Mwezi wa Ramadhani) ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.] [Al-Baqara:183]

Na dalili ya Hijja ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:

[Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.] [Al 'Imran:97


SHEREHE YA KITABU USUULU THALATHA 01



SHEREHE YA KITABU USUULU THALATHA 02



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487167
TodayToday273
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 46

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e572c3975b21002450911735284524
title_676e572c3984618995593421735284524
title_676e572c399295117024941735284524

NISHATI ZA OFISI

title_676e572c3b06411153331631735284524
title_676e572c3b1584312109401735284524
title_676e572c3b23c15740847021735284524 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com