SOMO LA FIQHI YA KUAMILIANA
Suala la tatu: Ushahidi katika Kuuza na kununuwa Biashara.
Inapendekeza katika uislamu kupatikane ushahidi katika kuuza na kununuwa wala si lazima, kwa mujibu wa neno lake Mwenyezi Mungu:
وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ} البقرة:282}
[Na shuhudieni munapouziana] [Suratul Baqra, Aya:282].
Kutokana na aya hii, Mwenyezi Mungu ameamrisha kupatikane ushahidi wakati wakuuziana; lakini maamrisho hayo ni ya kupendekeza wala si ya kulazimishwa, kwa dalili ya aya nyingine pindi aliposema:
فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ} البقرة:283}
[Na kama mmoja wenu ameweka amana na mwengine basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake.] [Suratul Baqra, Aya:283].
Amrisho lililotokana na aya hiyo ni amrisho la uongozi; ili kupatikane uthibitisho na maslahi.
Imepokewa na Amara Bin Khuzeima, akipokea kutoka kwa babake mdogo, akisimulia khabari itokayo kwa Mtume ﷺ kuwa [amenunua farasi kutoka kwa beduwi (mwarabu) na hakuwa na uthibitisho na hapo kuna jopo la watu walimuendea beduwi kutaka kumnunua farasi na hawakujua kuwa tayari mtume amekwisha kumnunua.]
Mafunzo yanayopatikana katika hadithi hii, lau kama ushuhuda ni jambo la lazima katika kuuzina Mtume ﷺ asingenunua farasi mpaka kupatikane shahidi kati yake na beduwi.
Pamoja na hayo, Maswahaba wake Mtume ﷺ walikuwa wakifanya biashara katika masoko bila ya uthibitisho wowote, wala haijapokewa kutoka kwao kuwa ushuhuda ni jambo la wajibu pale unapotaka kuuza au kununuwa.
Kuuza na kununuwa ni jambo hufanyika mara kwa mara katika masoko na lau ingelazimika kupatikane ushuhuda na uthibitisho baina ya watu ingepelekea kupatikana kwa mashaka kati yao.
Mbali na hayo, kama bidhaa ni yenye thamani na haikupatikana wakati huo wa kufanya biashara basi inawajibika kupatikane ushahidi; ili utumike kwa siku zifuatazo panapotokea ikhitilafu kati ya Muuzaji na Mnunuzi.
Today | 894 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.