Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


KIWANGO CHA KUTOLEWA ZAKA YA FITRI

Pishi moja na [Pishi ni sawa na kilo mbili na gramu arubaini (2.040 grms).]. kwa kila mtu, na kiwe ni chakula cha binadamu (kula) kama mchele, na tende, na ngano, kwa Hadith ya Abu Saii’d Alkhudhry radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema:

 

كنا نُخْرِجُ في عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم يوم الفطر صاعاً من طعام]     رواه البخاري]

 

[Ilikuwa tunatoa katika wakati wa Mtume ﷺ siku ya Fitri pishi moja ya chakula].

Na akasema: “Na kilikuwa chakula chetu ni Shayir (aina ya nafaka), na zabibu, na aqitwu (Maziwa yaliyokaushwa). na tende) [Imepokewa na Bukhari]..

Na pishi ni sawa na 3.25kg kulingana na dhehebu la hanafia, ama jumhuri ya wanavyoni ni sawa na 2.040kg.

Na hukadiriwa vile vile kwa kujaza mkono mara nne kwa mwanamume wasitani

 

WANAOSTAHIKI KUPEWA ZAKA YA FITRI.

Inatolewa Zaka ya Fitri kwa yale makundi manane ambayo kwamba yanapewa Zaka, kwa maana (Zaka ya Fitri) ipo ndani ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ      التوبة:60

 

[Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.]   [At-Tawbah: 60]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668170
TodayToday858
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 19

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6866b8f60dfb0417022811751562486
title_6866b8f60e09020881867881751562486
title_6866b8f60e15c21349124931751562486

NISHATI ZA OFISI

title_6866b8f60f53417152952091751562486
title_6866b8f60f60e10856134941751562486
title_6866b8f60f6e220241644031751562486 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com