SOMO LA FIQHI
HIKMA YA KUTOA ZAKA YA FITRI.
1. Kumsafisha aliyefunga kutokana na mambo ya upuzi na uchafu, kama ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas asema:
فرض رسول الله صلى الله عليه وسلم زكاة الفطر طهرة للصائم من اللغو والرفث، وطعمة للمساكين] رواه أبوداود]
[Amefaradhisha Mtume ﷺ Zaka ya Fitri kwa aliyefunga ili kumsafisha kutokana na upuzi na uchafu na ni chakula cha masikini] [Imepokewa na Abu Daud.].
Na hii ni kwamba aliyefunga mara nyingi haepukani na michezo, na maneno ya upuzi, na mambo yasiyo na faida katika maneno, basi ikawa hii Zaka inamsafisha aliyefunga kwa aliyoyafanya katika matamshi haya yaliyoharamishwa, au yaliyochukizwa kufanywa, ambayo kwamba yanapunguza thawabu za matendo, na kuharibu saumu.
2. Masikini na mafakiri kupata nafasi nzuri ya kimahitaji siku ya Idd ili kuepukana na kuomba ambako kuna udhalilifu na unyonge siku ya Idd, jambo hili (Zaka fitri) litawafanya wawe na furaha na bashasha, ili washirikiane na watu wengine katika kufurahia Idd.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.