Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


MAANA YA KHOFU

Khofu ni neno la Kiarabu ambalo hutumika kwa maana ya aina maalumu ya kiatu chenye umbo la soksi.Viatu hivi vinaweza kuwa ni vya ngozi au malighafi nyingine ifananayo na ngozi kama vile kitambaa kigumu.

Mojawapo ya misingi iliyojengewa sheria ya Kiislamu ni Wepesi.Siku zote uislamu huwatakia wepesi na urahisi wafuasi wake katika utendaji na utekelezaji wao wa ibada na matendo yao ya maisha ya kila siku.Ni kwa kuuzingatia msingi huu ndipo hutaweza kukuta hata mara moja uislamu umeweka sheria isiyotelelezeka.

Mwenyzi Mungu Mtukufu anasema:

 

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ}   الحج:78}

 

[Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini]      [Suratul Hajj:78]

Kwa sababu huu Uislamu umemjuzishia na kumruhusu muislamu kupakaza maji juu ya khofu badala ya kuosha miguu wakati wa kutawadha kwa masharti makhususi tutakayoyaona hapo baadae.

Na Ruhusa hii ni kwa wanamume na wanawake pamoja na itatumika mtu awapo safarini au mjini. 

Kupakaza maji juu ya khofu kumethibiti katika suna tukufu ya Bwana Mtume ﷺ.

Miongoni mwa hadithi zilizothibiti katika mas'ala haya ni Hadithi hizi zifuatazo:

 

1. Imepokelewa na Al Mughyrah Ibn Shu’ubah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema:

 

كُنْتُ مَع النّبيِّ - صلى الله عليه وسلم ، فَتَوَضَّأَ، فَأَهْوَيْتُ لأنْزِعَ خُفّيْهِ، فَقَالَ: دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ، فمَسَحَ عَلَيْهِمَا]   متفق عليه]

 

Nilikuwa pamoja na Mtume ﷺ Akatwadha nikaporomoka (nikainama) ili nimvue khofu zake, mtume akasema: [Ziache, kwani mimi nimezivaa il hali (miguu) ikiwa twahara, Akapakusa juu yake]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

2. Hadithi iliopokelewa na Anas Rahi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:

 

إذا توضأ أحدكم ولبس خفيه فليصل فيهما وليمسح عليهما ،ثم لا يخلعهما إن شاء إلا من جنابة]    رواه الدارقطني]

 

[Atakapotawadha mmoja wenu , kisha akavaa khofu. (Atakapotawadha tena) basi na apakaze maji juu yake (hizo khofu) na wala asizivue akitaka (kufanya hivyo) ila akipatwa na janaba.]       [Imepokea na  Al Daaruqutwiy]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

8355446
TodayToday562
Highest 09-30-2026 : 21356
US
Guests 111

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6ac8e0b433f8620552394411791549620
title_6ac8e0b433fe820658467991791549620
title_6ac8e0b43404318285675701791549620

NISHATI ZA OFISI

title_6ac8e0b44a93c2647308041791549620
title_6ac8e0b44a98d9583509111791549620
title_6ac8e0b44a9ea4582312111791549620 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

Go to top
UongofuUongofu.com