SOMO LA FIQHI
1. Kuswali kwa kutayamamu, iwapo haiwezekani kutumia maji, ni bora kuliko mtu kuswali na huku amejizuia mkojo au choo.
2. Inafaa kutayamamu kwenye ukuta au mswala na mfano wa hivyo, iwapo kuna mchanga au vumbi juu yake.
3. Yafaa kwa mwenye kutayamamu kuswali, kwa tayamamu moja, swala atakazo za faradhi na za sunna, iwapo bado hajatangukwa na tayamumu yake.
4. Yafaa kwa mwenye kutawadha kumfuata mwenye kutayamamu, kwa kuwa Mtume ﷺ alimkubalia ‘Amr bin al-’Asw Radhi za Allah ziwe juu yake alipowaswalisha wenzake hali ya kuwa ametayamamu kwa ajili ya baridi kali [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
5. Mwenye kutayamamu na akaswali, kisha akapata maji kabla ya wakati kutoka, hatairudia ile swala. Abu Said al-Khudri t amepokewa akisema:
خَرَجَ رَجُلَانِ في سَفَرٍ، فَحَضَرَتِ الصَّلَاةُ وَلَيْسَ مَعَهُمَا مَاءٌ، فَتَيَمَّمَا صَعِيدًا طَيِّبًا، فَصَلَّيَا، ثُمَّ وَجَدَا الْمَاءَ في الْوَقْتِ، فَأَعَادَ أَحَدُهُمَا الصَّلَاةَ وَالْوُضُوءَ، وَلَمْ يُعِدِ الآخَرُ، ثُمَّ أَتَيَا رَسُولَ اللهِ ﷺ فَذَكَرَا ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ ﷺ لِلَّذِي لَمْ يُعِدْ: أَصَبْتَ السُّنَّةَ، وَأَجْزَأَتْكَ صَلَاتُكَ، وَقَالَ ﷺ لِلَّذِي تَوَضَّأَ وَأَعَادَ: لَكَ الأَجْرُ مَرَّتَيْنِ رواه أبوداود
[Walitoka watu wawili safarini, wakati wa Swala ukaingia na wao hawana maji, wakakusudia ardhi nzuri wakatayamamu na wakaswli, kisha wakapata maji ndani ya wakati, mmoja wao akarudia swala na udhu, na yule mwingine asirudie. Kisha wakamjia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ wakamuelza hayo, akasema kumwambia yule ambaye hakurudia “Umepata Sunna na Swala yako imekutosheleza” na akmwambia yule aliyetawadha na akarudia “Wewe una thawabu mara mbili”] [Imepokewa na Abu Daud.]
6. Mwenye kutayamamu kisha akapata maji kabla ya kuswali au katikati ya Swala, itamlazimu kujitwahirisha kwa maji, kwa kauli ya Mtume ﷺ:
إِنَّ الصَّعِيدَ الطَّيِّبَ طَهُورُ الْمُسْلِمِ، وَإِنْ لَمْ يَجِدِ الْمَاءَ عَشْرَ سِنِينَ، فَإِذَا وَجَدَ الْمَاءَ فَلْيُمِسَّهُ بَشَرَتَهُ، فَإِنَّ ذَلِكَ خَيْرٌ] رواه الترمذي]
[Hakika ardhi nzuri ni twahirisho kwa Muislamu, hata kama hatapata maji miaka kumi. Atakapopata maji basi ayatumie kwenye ngozi yake ya mwili, kwani hilo ni kheri] [Imwpokewa na Tirmidhi]
7. Hakuna cha kumfunga Muislamu na Swala wala kuichelewesha wakati wake. Akitoweza kutumia maji au asipoyapata, atatayamamu, akielemewa na kutayamamu pia, basi ataswali bila twahara.
8. Mwenye kukosa vitwahirisho viwili (maji na mchanga) ataswali wakati ukiingia bila ya twahara wala haimlazimu kurudia, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ} التغابن:16}
[Mcheni Mwenyezi Mungu mnavyoweza] [64: 16]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.