SOMO LA FIQHI
Ili upangusaji juu ya khofu usihi kisheria ni lazima yapatikane sharti kadhaa kama zilivyotajwa na Wanachuoni. Miongoni mwa sharti muhimu kabisa ni hizi zifuatazo:-
1.Kuzivaa baada kujitwahirisha kikamilifu.
Kwa Hadithi iliopokelewa na Al Mughirah Radhi za Allah zawe juu yake asema:
كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ ﷺ فِي سَفَرٍ فَأَهْوَيْتُ لِأَنْزِعَ خُفَّيْهِ، فَقَال: دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ. فَمَسَحَ عَلَيْهِمَا] متفق عليه]
[Nilikuwa na Mtume ﷺ safarini, nikaporomoka ili kuzivua khofu zake, akasema: [Ziache, kwani mimi nimezivaa katika hali ya utwahara akapukusa juu yake] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
2. Ziwe ni zenye kusitiri miguu mpaka kwenye vifundo
zikiwa hazikusitiri Miguu mpaka kwenye vifundo viwili haifai kupangusa juu ya khofu hizo.
3. Ziwe zimetengezwa kwa vitu vilivyo twahara.
Ikiwa khofu zimetengenezwa kwa vitu vya Najisi basi haifai kupangusa juu yake.
4. Ziwe zinafaa kutumiwa na zisiwe ni miongoni mwa vitu haramu kama hariri kwa wanaume.
5. Kule kupukusa kuwe ndani ya muda uliowekwa. Kwani Mtum ﷺ aliweka muda maalumu wa kupukusa usiku na mcha kwa mkazi na siku tatu kwa msafiri. Haifai kupitisha muda huo.
6. Kupukusa kuwe kwenye kujitwahirisha kutokana twahara ndogo, kama kutangukiwa na udhu na sio tukio kubwa la ukosefu wa twahara. Imepokewa na Swafwan bin Assal Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:
كَانَ رَسُولُ اللهِ ﷺ يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا مُسَافِرِينَ أَنْ نَمْسَحَ عَلَى خِفَافِنَا، وَلَا نَنْزِعَهَا ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ مِنْ غَائِطٍ، وَبَوْلٍ، وَنَوْمٍ، إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ» رواه البخاري
[Alikuwa Mtume ﷺ akituamrisha tukiwa safarini tupukuse khofu zetu, na tusizifue siku tatu, kwa kwenda haja kubwa, kukojoa na kulala isipokuwa kutokana na janab] [Imepokewa na Bukhari.]
Yaani mwenye janaba ni juu yake azivue khofu mbili kwa kuoga kisha azivae mara nyingine.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.