SOMO LA FIQHI
Tayamamu hutenguka na kubatilika kwa kupatikana mambo yafuatayo :
1. Kupata maji baada ya kuyakosa. Hii ni kwa sababu kutayamamu ni badala ya maji, kwa hivyo itakapopatikana asili nayo ni maji hubatilika badala (tayamamu).
Kwa mujibu wa hadithi iliyopokelewa na Abu Dharri Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa mwenyezi Mungu ﷺ amesema :
إِنَّ الصَّعِيدَ الطَّيِّبَ طَهُورُ المُسْلِمِ، وَإِنْ لَمْ يَجِدِ المَاءَ عَشْرَ سِنِينَ، فَإِذَا وَجَدَ المَاءَ فَلْيُمِسَّهُ بَشَرَتَهُ، فَإِنَّ ذَلِكَ خَيْرٌ] رواه أبوداود]
[Hakika mchanga ulio safi ni tahara ya Muislamu hata kama hakupata maji kwa miaka kumi. Atakapoyapata maji basi na ajitwaharishe nayo kwani kufanya hivyo ndio bora] [Imepokewa na Abuu Dawud.]
Hadithi hii inafahamisha kubatilika kwa tayamamu kwa kupatikana maji.
2. Mambo yote yanayotenguka na udhu tuliyoyataja katika mlango wa udhu.
3. Kuondokewa na udhuru wa kutayamamu uliowekwa na Sheria, kama ugonjwa na mfano wake.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.