Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Kumesuniwa katika kutayamamu mambo kadhaa, miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo :-

1. Kunasuniwa katika tayamamu yale yote ambayo ni suna katika udhu. Kuanzia na :

a. Kupiga “Bismillah” mwanzo wa kutayamamu

b. Kuanza kupangusa mkono wa kulia.

c. Kuomba dua baada ya kutayamamu.

2. Kupiga Ardhi kwa mara ya Pili.

 

عن عمار بن ياسر أنهم حين تيمموا مع رسول الله صلى الله عليه وسلم فأمر المسلمين فضربوا بأكفهم التراب ولم يقبضوا من التراب شيئا ، فمسحوا بوجوههم مسحة واحدة ، ثم عادوا فضربوا بأكفهم الصعيد مرة أخرى ، فمسحوا بأيديهم     رواه أبوداود وإبن ماجة

 

Imepokelewa hadithi na Ammaar Ibn Yaasir Radhi za Allah ziwe juu yake [Kwamba wao walitayamamu wakiwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu  ﷺ akawamrisha Waislamu

Wakapiga viganja vyao mchangani, wala hawakuchukua mchanga wowote kisha wakapangusa nyuso zao mara moja.Halafu wakarudia tena kupiga viganja vyao mchangani mara nyingine, wakapangusa mikono yao.]   [Imepokewa na Abuu Daawud na Ibnu Maajah]

3. Kutapanya vidole wakati wa kupiga viganja juu ya mchanga na kueneza uso kwa pigo moja tu la mchanga na kuieneza mikono kwa pigo jingine.

4. Kupunguza vumbi kwa kupuliza viganja baada ya kupiga.

Suna hii inapatikana katika hadithi iliyopokelewa na Swahaba Ammar Ibn Yaasir Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia 

 

[إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ أَنْ تَقُولَ بِيَدَيْكَ هَكَذَا ، ثُمَّ ضَرَبَ بِيَدَيْهِ الأَرْضَ ضَرْبَةً وَاحِدَةً ، ثُمَّ مَسَحَ الشِّمَالَ عَلَى الْيَمِينِ وَظَاهِرَ كَفَّيْهِ وَوَجْهَهُ]

 

[Hakika si vinginevyo inakutosha kufanya hivi”. Akapiga (Mtume) viganja vyake juu ya ardhi pigo moja kisha akapangusa Mkono wa kushoto Mkono wa kulia na kwa akapangusa kwa (viganja hivyo) Uso wake]

Na katika riwaya nyingine ya Bukhari:

 

[وفي رواية للبخاري : [ ونفخ فيهما

 

[Na akapulizia ndani yake (viganja)]   halafu akapangusa kwa (viganja) hivyo.                                                                                                                                                   


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487228
TodayToday334
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 70

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5ab82a64f10914339581735285432
title_676e5ab82a74a19795092731735285432
title_676e5ab82a8473187796501735285432

NISHATI ZA OFISI

title_676e5ab82bff616632213481735285432
title_676e5ab82c0eb18362659641735285432
title_676e5ab82c1de5163565611735285432 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com