SOMO LA FIQHI
NAMNA YA KUTAYAMAMU.
1. Aupige mchanga kwa mikono yake pigo moja.
2. Kisha aipulize kupunguza vumbi.
3. Kisha apanguse uso wake kwa hiyo mikono mara moja.
4. Kisha apanguse upande wa nje wa wa vitanga vya mikono. Apanguse sehemu ya nje ya kitanga cha mkono wa kulia kwa sehemu ya ndani ya kitanga cha mkono wa kushoto, kisha nje ya kitanga cha mkono wa kushoto kwa sehemu ya
Na dalili ya namna ya kutayamamu ni hadithi ya Ammar Radhi za Allah ziwe juu yake
أن النَّبِيَّ ﷺ ضَرَبَ بِكَفَّيْهِ الْأَرْضَ، وَنَفَخَ فِيهِمَا، ثُمَّ مَسَحَ بِهِمَا وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ] متفق عليه]
[Kwamba Mtume ﷺ alipiga ardhi kwa vitanga vyake viwili vya mkono, akavipuliza kisha akapangusa uso wake na vitanga vyake kwavyo] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
FARADHI ZA KUTAYAMAMU.
1. Kutia nia.
2. Kupangusa uso.
3. Kupangusa vitanga vya mikono.
4. Kufuatanisha: aanze kupangusa uso kisha vitanga viwili vya mikono.
5. Kufuliliza: Apanguse mikono miwili baada ya kupangusa uso papo kwa papo.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.