SOMO LA FIQHI
1. YANAPOKOSEKANA MAJI
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا} المائدة:6}
[Na mkitopata maji tayamamuni] [5: 6].
Na mtu haambiwi kuwa amekosa maji iwapo hakuyatafuta.
2. KUSHINDWA KUYATUMIA MAJI
Kama mgonjwa au mkongwe asiyeweza kutembea, na akawa hana wa kumsaidia kutawadha.
3. WAKATI WA KUCHELEA MADHARA KWA KUTUMIA MAJI
Miongoni mwa hayo:
a) Mgonjwa ambaye angeyatumia maji ugonjwa wake utazidi.
b) Mtu aliye mahali penye baridi kali na asiwe na kitu cha kupasha maji moto na akawa na yakini lau ataoga atapatikana na ugonjwa.
Hii ni kwa hadithi iliyothubutu kuwa Mtume ﷺ alimkubalia ‘Amr bin al-’Asw alipowaswalisha wenzake hali akiwa ametayamamu kwa sababu ya baridi kali [Imepokewa na Abu Daud.].
c) Awapo mahali mbali na hana maji isipokuwa kidogo ambayo anayahitajia kwa kunywa na hawezi kuleta mengine.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.