SOMO LA FIQHI
MAANA YA KUTAYAMAMU
Kutayamamu kilugha: Ni Kukikusudia kitu na kukielekea
Ama Maana yake kisheria: Ni Kupukusa uso na viganja vya mikono miwili kwa ardhi Twahara kwa nia ya kujitwahirisha
HUKMU YA KUTAYAMAMU
Inapasa kutayamamu yakikosekana maji au ikawa haiwezikani kuyatumia kwa jambo linalolazimu utwahara kama vile Swala. na kutayamamu kunapendekezwa katika kufanya jambo linalopendekezwa kama vile kusoma Qur'ani.
DALILI ZA KUTAYAMAMU
Kutayamamu kumethibiti katika Qur-ani Tukufu, Sunna na Ijmaa ya Wanachuoni.
Dalili ya Kutayamamu katika Qur'ani.
1. Mwenyezi Mungu ﷻ Anasema:
فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ} النساء:43}
[Mkitopata maji kusudieni ardhi nzuri, mpanguse nyuso zenu na mikono yenu ] [4:43]
Ama Dalili yake katika Sunna.
2. Amesema Mtume ﷺ:
أعطيت خمسا ، لم يعطهن أحد من الأنبياء قبلي : نصرت بالرعب مسيرة شهر ، وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا ، فأيما رجل من أمتي أدركته الصلاة فليصل رواه البخاري
[Nimepewa mambo matano hakuna aliyepewa kabla yangu: Nimenusuriwa kwa kitisho masafa ya mwezi, nimefanyiwa ardhi kuwa ni mahali pa kuswali na pa kujitwahirishia: kwani yoyote katika umma wangu atakayeingiliwa na kipindi cha Swala na aswali] [Imepokewa na Bukhari.].
Ama Ijmaa, wanazuoni wote wamekogomana na kukubaliana kuwa tayamamu imefanywa kuwa ni sheria, itumike badala ya ya udhu na josho katika hali na mazingira maalum yaliyobainishwa na sheria.
HEKIMA YA SHERIA KUWEKA KUTAYAMAMU
1. Kuwasahilishia umma wa Mtume Muhammad ﷺ
2. Kuepusha madhara yanayosababishwa na utumiaji maji katika hali ya ugonjwa, na baridi kali na mfano wa hayo.
3. Kudumisha mafungamano ya ibada yasikatike kwa kukosekana maji, au kutoweza kuyatumia
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.