Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


MAANA YA HEDHI

Hedhi katika lugha ya kiarabu, maana yake ni Kuchurizika.

Ama hedhi kwa mtazamo wa sheria:

"Ni damu inayotoka kwenye uzao wa mwanamke katika muda maalumu bila ya sababu"

yaani damu hii ni katika jumla ya maumbile ya mwanamke, mwanamke kaumbwa hivyo kwa lengo maalum.

Damu hii kutoka ndani kabisa ya tumbo la uzazi kila mwezi baada ya mwanamke kutimiza kwa uchache umri wa miaka tisa.

Namna ya damu ya hedhi ilivyo
Ni nyeusi kama kwamba imechomeka kwa weusi wake mwingi, yaumiza, ina harufu mbaya, mwanamke akiwa nayo huhisi joto lingi mwilini.

DALILI YAKE

Dalili na ushahidi juu ya kuwa hadhi huwajibisha josho la kisheria ni Qur'ani Tukufu na Sunnah za Bwana Mtume .

Ama katika Qur'ani ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ

 

[Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.]   [Al Baqara:222]

Ama dalili yake katika sunnah ni kauli ya Bwana Mtume kumwambia Fatmah Bint Abiy Hubayshi Allah amuwiye radhi-:

 

فإذا أقبلت الحيضة فاتركي الصلاة . فإذا ذهب قدرها ، فاغسلي الدم عنك وصلي ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Itapokujia hedhi , basi acha kuswali na itakapomalizika (kutoka) basi ikoshe damu (twaharisha) na uswali]      [Imepokewa na Bukhaariy na Muslim.]

MIAKA YA HEDHI 

Hakuna miaka maalumu ya kuanzia hedhi, kwani inatafautiana kulingana na tabia ya mwanamke, na mazingira yake na hewa yake, wakati wowote mwanamke aonapo damu ya hedhi, basi yeye ameingia hedhini.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785144
TodayToday145
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 27

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a952b9b751c6713458781755927225
title_68a952b9b760514911660261755927225
title_68a952b9b76f316474188071755927225

NISHATI ZA OFISI

title_68a952b9b8c8f15090971461755927225
title_68a952b9b8d7213283904381755927225
title_68a952b9b8e5b5790996361755927225 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 12 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com