Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Kuoga kunakopendekezwa

1. KUOGA KWA AJILI YA SWALA YA IJUMAA

Kwa kauli ya Mtume :

 

من توضأ، فبها ونعمت، ومن تغسل فالغسل أفضل]    رواه أبوداود]

 

[Mwenye kutawadha kwa ajili ya kwenda Ijumaa, hilo ni jambo zuri, na mwenye kuoga, basi kuoga ni bora]    [Imepokewa na Abu Daud.]

2. KUOGA WAKATI WA KUHIRIMIA KWA AJILI YA UMRA NA HIJA.

Imepokewa kutoka kwa Zaid bin Thabit kwamba yeye alimuona Mtume :

 

تَجَرَّدَ لإِهلالِهِ وَاغتَسَلَ]   رواه الترمذي]

 

[Akijiondoa na nguo za kawaida kwa ibada ya Hija na akaoga]   [Imepokewa na Tirmidhi]

3. KUOGA BAADA YA KUOSHA MAITI.    

 

مَن غَسَّلَ مَيتًا فَلْيَغتَسِلْ]    رواه أحمد والترمذي]

 

Kwa neno la Mtume ﷺ: [Mwenye kuosha maiti aoge]     [Imepokewa na Ahmad na Attirmidhiy.]

4. KUOGA BAADA YA KILA TENDO LA NDOA.

Imepokewa na Abu Rafi'i radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ:

 

طَافَ ذَاتَ يَوْمٍ عَلَى نِسَائِهِ يَغْتَسِلُ عِنْدَ هَذِهِ وَعِنْدَ هَذِهِ ، قَالَ قُلْتُ : لَهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَا تَجْعَلُهُ غُسْلًا وَاحِدًا قَالَ :  هَذَا أَزْكَى وَأَطْيَبُ وَأَطْهَرُ     رواه أبوداود

 

[Siku moja aliwapitia wake zake, na alikuwa akioga baada ya kumaliza kwa huyu na kwa yule. Mpokeaji asema: (Nikamwambia”Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! usiuoge mara moja? Akasema ﷺ  [Hili ni safi zaidi, bora zaidi na twahara zaidi]         [Imepokewa na Abu Daud.]

 

MAKATAZO

1- kuchelewesha kuoga janaba mpaka utoke wakati wa Swala.

2- kwa mwanamke aliyetwahirika na hedhi kuacha Swala ya wajibu. Na lau atwahirika kabla ya kutoka wakati wa adhuhuri kwa kadiri ya rakaa moja, basi itampasa aoge na aswali adhuhuri. Mtume amesema:

 

من أدرك من الصبح ركعة قبل أن تطلع الشمس فقد أدرك الصبح ومن أدرك ركعة من العصر قبل أن تغرب الشمس فقد أدرك العصر]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Mwenye kuwahi rakaa moja ya asubuhu kabla ya kuchomoza jua, basi amewahi Swala ya asubuhi. Na mwenye kuwahi rakaa moja ya alasiri kabla ya jua kuzama, basi amewahi Swala ya alasiri]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487046
TodayToday152
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 58

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e53a2bd81c14195762271735283618
title_676e53a2bd9068499708331735283618
title_676e53a2bd9ea14918936671735283618

NISHATI ZA OFISI

title_676e53a2bef5d4821974411735283618
title_676e53a2c968610576995261735283618
title_676e53a2c978c14979965991735283618 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com