Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifanya twahara kuwa ni sheria na kuwafaradhishia waja wake kwa sababu twahara humfanya muislamu aishi maisha ya unadhifu na utakasifu.

Humfanya awe mtakasifu wa mwili, nadhifu wa mavazi na mahala aishipo.

Utakasifu na unadhifu huu humjengea afya njema na mwenendo mzuri kitabia.

Usafi huu wa nje dhahiri ni barabara na chombo cha kumfikisha katika usafi na utakasifu wa ndani batini ambao humfanya kuwa ni mtakasifu wa moyo, mwenye kauli nzuri laini na nafsi iliyosalimika na husuda, udanganyifu na tabia mbaya zote kwa ujumla.

Muislamu wa kweli ni yule aliyetakasika nje na ndani wakati wote khasa khasa wakati wa kutekeleza ibada, hii ndio sababu Bwana Mtume akatuambia:

 

الطهور شطر الإيمان]   رواه مسلم]

 

[Twahara ni nusu ya Imani]   [Imepokewa na Muslim]

Kwa sababu imani ya uhakika imefungamana na kutwahirika ndani na nje,Moyo kutohirika na chuki,na kiburi na Hasad.Na mwili kutohirika na uchafu na najisi ndio ikahisabiwa kuwa tohara ni nusu ya Imani.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487200
TodayToday306
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 42

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5ab82a64f10914339581735285432
title_676e5ab82a74a19795092731735285432
title_676e5ab82a8473187796501735285432

NISHATI ZA OFISI

title_676e5ab82bff616632213481735285432
title_676e5ab82c0eb18362659641735285432
title_676e5ab82c1de5163565611735285432 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com