SOMO LA FIQHI
Suali: Vipi hutahirishwa Ardhi iliyonasika ?
Jawabu: Ardhi iliyonasika hutwahirishwa kwa kuiondoa ile najisi au kwa kwa kuimiminia Maji.
Kama ilivyo kuja Katika hadithi ya mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume ﷺ: Alisema kuwambia Maswahaba wake:
دَعُوهُ وَهَرِيقُوا عَلَى بَوْلِهِ سَجْلًا مِنْ مَاءٍ أَوْ ذَنُوبًا مِنْ مَاءٍ] رواه البخار ومسلم]
[Muwacheni na mwageni kwenye mkojo wake ndoo ya maji] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na iwapo najisi ni majimaji ya kutiririka kisha ikakauka basi kwa hivyo huwa ishatwahirika kulingana na hadithi ya Abuu Qilaabah Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:
إذَا جَفَّتِ الأَرْضُ فَقَدْ زَكَتْ [ زكت: طهرت]ٍ رواه البخاري]
[Ardhi ikikauka huwa imetwahirika”] [Imepokewa na Bukhari.]
Suali: Maji yalionajisika hutwahiriswa namna gani?
Jawabu: Maji yalionajisika hutwahirika kwa namna mpili:
1. Hutwahirika kwa kuongeza maji mengi ndani yake mapaka ikaondoka athari ya najisi.
2. Pia yanatwahirika kwa kuyasafisha kwa njia za kiteknolojia za kisasa.
Suali: Nguo ilio ingia najisi hutwahirika namna gani?
Jawabu: nguo ilio ingia najisi hutwahirika kwa kuoshwa kwa maji mpaka Athari ya najisi iondoke kwa kuondoka rangi yake na harufu yake,lakini inapo shindikana kutoka kwa rangi yake husamehewa kwa sharti iwe harufu ya najisi imeondoka.
Suali: Matandiko kama vile mazulia na mfano wake yanapo najisikia hutwahirishwa namna gani?
Jawabu: Kuyatwahirisha matandiko yalio najisika,kama vile mazulia na mfano wake,
Huoshwa kwa maji mpaka ya kaondoka athari ya najisi na ikiwa najisi imeganda basi hukangurwa kisha kusafishwa kwa maji, au kwa visafishaji vya kisasa,mpaka najisi iondoke.
Suali: Vipi hutwahirishwa ngozi ya mnyama anaeliwa?
Jawabu: Hutwahirishwa ngozi ya mnyama anaeliwa kwa kuitia rangi kwa kauli yake Mtume ﷺ:
إِذَا دُبِغَ الإِهَابُ فَقَدْ طَهُرَ] رواه مسلم]
[Ngozi ikitiwa rangi huwa imetwahirika] [ Imepokewa na Muslim.]
Na dibaagh ni kutengeneza ngozi kwa baadhi ya madawa mpaka zilainike na uvundo wake uondoke. Ama mnyama anayeliwa awapo si mfu na akawa amechinjwa kwa njia ya kisheria, basi ngozi yake ni twahara
Kwa Yule mnyama ambae haiwi halali kuchinjwa kwake ngozi yake haitotwahirika kwa kukaushwa hata kama katika uhai wake alikuwa twahara.
Suali: Vipi hutahirishwa mkojo wa mtoto wa kiume na wakike ambae hajakula?
Jawabu: Hutwahirisha mkojo wa mtoto wa kike kwa kuoshwa na Maji.Ama mkojo wa mtoto wa kiume, inatosha kunyunyiza maji juu yake, kwa kauli yake Mtume ﷺ:
يُغْسَلُ مِنْ بَوْلِ الْجَارِيَةِ، وَيُرَشُّ مِنْ بَوْلِ الْغُلَامِ] رواه أبو داود]
[Mkojo wa mtoto wa kike huoshwa, na mkojo wa mtoto wa kiume hunyunyizwa maji] [Imepokewa na Abu Daud.]
Suali: hutwahirishwa vipi chombo kilichoramba na Mbwa?
Jawabu: Chombo kilichorambwa na Mbwa Huoshwa mara saba, na mara ya kwanza yake huoshwa na mchanga, kwa kauli yake Mtume ﷺ:
طَهُورُ إِنَاءِ أَحَدِكُمْ إِذَا وَلَغَ فِيهِ الْكَلْبُ أَنْ يَغْسِلَهُ سَبْعَ مَرَّاتٍ أُولَاهُنَّ بِالتُّرَابِ ] رواه مسلم]
[Utwahara wa chombo cha mmoja wenu iwapo mbwa amekiramba ni kukiosha mara saba, mara ya kwanza yake ni kwa mchanga] [ Imepokewa na Muslim]
Suali: Madhii na Wadii yanapo ingia kwenye nguo hutwahirishwa namna gani?
Jawabu: Kuyatwahirisha Madhii na Wadii
Kwanza mtu anapo tokwa na Madhi na wadii analzimika kuosha dhakari yake na atatawadha, kwa kauli yake Mtume ﷺ katika hadithi ya Ali bin Abii Twalib:
توضأ واغسل ذكرك] رواه البخاري]
[Tawadha na uoshe dhakari yako] [ Imepokewa na Bukhari.]
Ama kuitwahirisha nguo, inatosha kunyunyiza maji mahali palipo na madhii au wadii, kwa hadithi ya Sahl bin Hanif kuwa yeye alimuuliza mtume ﷺ:
يا رسول الله فكيف بما يصيب ثوبي منه؟ قال: "يكفيك أن تأخذ كفاً من ماء فتنضح به ثوبك حيث ترى أنه أصاب منه". رواه الترمذي وأبو داود وقال الترمذي حديث حسن صحيح
[Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nguo yangu ikiiingiwa na chochote katika vitu hivyo itakuwaje?” Akasema: (Inakutosheleza utie maji kwenye kitanga cha mkono uyamimine nguoni mwako mpaka uone kwamba yameviondoa] [Imepokewa na Tirmidhiy na Abu Daud na akasema Tirmidhi ni hadithi Hasan swahihi]
Na wamenda badhi ya Wanchuoni kuwa Huoswa kwa Maji ila kwa yule ambae yuwatokwa sana na Madhii kama hali aliyokuwa nayo swahaba sahal bin hanif.
Suali: Damu ya Hedhi ikiingia kwenye ngou hutahishwa namna gani ?
Jawabu: Nguo inapo ingia Damu ya hedhi au damu yanifasi ikiwa imeganda hukangurwa kisha huoshwa kwa Maji,kama vile Mtume ﷺ alipo mwambia Asmaa ikangure kisha uoshe kwa Maji.
na inapo oshwa kwa maji na kuondoka Athari ya damu itatosheleza, ama ikiwa athari ya damu itabakia baada ya kutumia visafishaji basi itakuwa imetwahirika na haidhuru kubakia Athari yake, kwa kauli yake Mtume ﷺ:
يكفيك الماء ولا يضرك أثره ] رواه أحمد وأبو داود]
[Yanakutosheleza maji, na athari yake haikudhuru] [Imepokewa na Abu Daud.]
Suali: Viatu vinapo ingia najisi hutwahirishwa namna gani?
Jawabu: Viatu vinapo ingia najisi na akawa mtu ataka kuswali navyo, basi atavisugua chini yake mpaka iondoke athari ya najisi, kwa kauli yake Mtume ﷺ:
إذا وطئ أحدكم بنعله الأذى، فإن التراب له طهور] رواه أبوداود]
[Mmoja wenu anapokanyaga uchafu kwa kiatu chake, basi mchanga unakitwahirisha] [Imepokewa na Abu Daud.]
Suali: Hutwahirika vipi Nguo ndefu ya Mwanamke ?
Jawabu: Mwanamke ikiwa amevaa hijabu ndefu na akapita kwenye sehemu kuna najisi iliokauka ikipakana na ukingo wa hijabu yake, basi inamtosheleza yeye atembee mahali twahara na ardhi itaitwahirisha, kwa kauli yake Mtume ﷺ
يطهره ما بعده] رواه أبوداود]
[Kitaitwahirisha kilicho baada yake] [ Imepokewa na Abu Daud.]
Lakini ikiwa najisi ni Maji maji kama vile maji ya mitaro,au kinyesi badhi ya wanachuoni wamesema kuwa nilazima kuoshwa kwa Maji.
Suali: Hutwahirishwa vipi Vyakula vikavu vilivyo ingia najisi?
Jawabu: Vinatwahirika kwa kuiondoa najisi na zile sehemu zilizo pambizoni mwa hivyo vyakula, na kinachosalia kitakuwa twahara, kwa ilivyothubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliulizwa kuhusu panya aliyeingia ndani ya samli, akasema:
ألقوها وما حولها وكلوه ] رواه البخاري]
[Vitupeni! Na vile vilivyo pambizoni mwakeviondoeni namule samli yenu] [ Imepokewa na Bukhari.]
Na chakula kikiwa ni majimaji hunajisika na haifai kutumia chakula hicho.
Suali: Vitu Vigumu kama Viyoo na Gilasi vinapo ingia najisi hutwahirishwa vipi?
Jawabu: Vitapanguswa mpaka iondoke athari ya najisi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.