SOMO LA FIQHI
KISIMAMO CHA MWANAMKE KATIKA SWALA
1. Wanaposwali wanawake kwa jamaa, lililo sunna ni asimame imamu wao kati ya safu yao na asiwatangulie.
2. Mwanamke husimama nyuma ya mwanamume iwapo mwanamume ni imamu wake. Na akiswali na wanaume basi atasimama nyuma ya safu.
3. Iwapo wanaume na wanawake wanaswali jamaa, sunna ni wawe nyuma ya wanaume. Na safu zao huwa ni kama safu za wanaume. Abu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema:
وَخَيْرُ صُفُوفِ النِّسَاءِ آخِرُهَا وَشَرُّهَا أَوَّلُهَا] والحديث رواه أحمد وأهل السنن الأربعة فهو حديث ثابت صحيح]
[Bora ya safu za wanawake ni zile zilizo nyuma ya safu, na shari ya safu za wanawake ni zile za mwanzo wake] [Imepokewa na Ahmad na wengineo.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.