SOMO LA FIQHI
ANAYESTAHIKI ZAIDI UIMAMU KWA MPANGILIO:
Kwanza: Msomi zaidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu: naye ni aliyekihifadhi zaidi na kuuzifahamu zaidi hukumu zake.
Pili: Mjuzi zaidi wa Sunna (mafundisho ya Mtume ﷺ: naye ni yule anayejua zaidi ya maana za hadithi zake na hukumu zilizomo ndani ya hizo hadithi.
Tatu: Mwenye kutangulia kugura (Hijra): Mwenye kutangulia kugura kutoka nchi ya kikafiri na kuenda nchi ya kisalmu. Naikiwa Hakuna hijra basi Mwenye kuhama machafu nakurudi kwa Mwenyezi Mungu.
Nne: Mkuu zaidi wa miaka: Hapa ni iwapo kuna kulingana katika hayo yaliyopita.
Na dalili ya haya yaliyotangulia ni hadithi iliyopokewa na Ibnu Mas’ud al-Answari Radhi za Allah ziwe juu yake alisema kwamba Mtume ﷺ alisema:
يَؤُمُّ الْقَوْمَ أَقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ اللَّهِ، فَإِنْ كَانُوا فِي الْقِرَاءَةِ سَوَاءً فَأَعْلَمُهُمْ بِالسُّنَّةِ، فَإِنْ كَانُوا فِي السُّنَّةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ هِجْرَةً، فَإِنْ كَانُوا فِي الْهِجْرَةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ سِلْمًا وفي رواية فَأَكْبَرُهُمْ سِنًّا ، وَلَا يَؤُمَّنَّ الرَّجُلُ الرَّجُلَ فِي سُلْطَانِهِ، وَلَا يَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إِلَّا بِإِذْنِهِ رواه مسلم
[Atawaongoza watu katika Swala msomi zaidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Wakiwa wamelingana katika usomi, basi mjuzi zaidi wa Sunna miongoni mwao. Wakiwa wamelingana katika ujuzi wa Sunna ni yule aliyewatangulia katika hijra (kugura), na iwapo wamelingana katika kugura, basi ni yule aliyewatangulia katika Uislamu na katika riwaya nyingine aliyemkubwa kwa umri, Na mtu asiwe Imamu wa mtu mwingine kwenye mamlaka yake, na asikaye nyumbani kwake kwenye maandalizi yake isipokuwa kwa ruhusa yake] [Imepokewa na Muslim.]
Na unazingatiwa mpango huu itakikanapo kumuweka imamu wa msikiti au katika jamaa ya watu wasiokuwa na imamu ratibu (naye ni imamu maalumu wa kuswalisha katika msikiti). Ama msikiti ukiwa na imamu ratibu au imamu akawa ni mwenye nyumba, au akawa ni mtawala, basi yeye atangulizwa mbele ya mwengine, kwa neno lake Mtume ﷺ:
وَلَا يَؤُمَّنَّ الرَّجُلُ الرَّجُلَ فِي سُلْطَانِهِ، وَلَا يَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إِلَّا بِإِذْنِهِ ] رواه مسلم ]
[Na mtu asiwe Imamu wa mtu mwingine kwenye mamlaka yake, na asikaye nyumbani kwake kwenye maandalizi yake isipokuwa kwa ruhusa yake] [Imepokewa na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.