Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi 


Mwenye kuswali anaruhusiwa kisheria kufanya baadhi ya mambo akiwa ndani ya swala, kwa sharti kwamba kuwe na dharura ya kufanya hivyo.

Anaruhusiwa kuyafanya mambo hayo katika hali hiyo ya dharura bila ya swala yake kubatilika. Mambo hayo ni kama yafuatavyo:-

1. Kutembea katika Swala kwa tukio muhimu kwa sharti ya kutogeuka upande wa kibla kama kufunguwa mlango kama alivyofanya Mtume kwa Hadithi aliyoipokea Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake Asema:

 

كان رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلَّم يصلِّي في البيت والبابُ عليه مغلق، فجِئتُ فاستفتحتُ، فمشى ففتح لي، ثم رجعَ إلى مُصلاَّ         أخرجه أبوداو والنسائي

 

[Mtume ﷺ alikuwa akiswali Nyumbani na mlango ulikuwa umefungwa nilikuja kuufungua,(nikashindwa) akaja kunifungulia kisha akarudi kwenye Mswala wake]   [Imepokewa na Abuu Daud na An Nasai]

2. Kubeba mtoto katika Swala

Amepokea Abuu Qatada Radhi za Alla ziwe juu yake amesema:

 

رأيتُ النبِيَّ صلَّى الله عليه وسلَّم يؤمُّ النَّاس، وعلى عاتقِه أمامةُ بنت زينب، فإذا ركَع وضَعها، وإذا رفع من السُّجود أعادَها   رواه البخاري ومسلم

 

[Nilimuona Mtume rehma na amani zimfike yeye akiswalisha watu,na (amembemba) kwenye mabega yake Umaamah bint Zaynab, Alikuwa ikirukuu akimuweka na ikiinika kutoka kwenye Sijda akimrudisha (kumbeba)]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

3. Kuuwa nyoka na n’nge katika Swala.

Mtume Ameamrisha kuuwa vyeusi viwili ndani ya Swala nyoka na nge   [Imepokewa na Abuu Daud na An Nasaai na Ibnu Maajah]

4. Kuzunguka katika Swala kwa dharura.

Amepokea  Jaabir  radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Mtume  aliposhikika na Ugonjwa Tuliswali Nyuma yake na yeye alikuwa amekaa akatuzungukia akatuona Tumesimama akatuashiria (kukaa) tukakaa]     [Imepkewa na Muslim na Abuu Daud]

Ama kuzunguka bila ya Dharura ni Makruhi kwa sababu ni kinyume na Unyenyekevu katika Swala.

5. Kulia katika Swala

Alikuwa [Mtume  wa Mwenyezi Mungu akiswali na kwenye kifua chake kuna Sauti kama sauti ya Chungu kwa ajili ya kulia]      [Imepokewa na Abuu Daud na An Nasai]

6. Kuleta tasbihi kwa wanaume na kupiga makofi kwa wanawake

Amesema Mtume ﷺ:

 

مَن نابَه شيءٌ في صلاته، فلْيُسبِّح؛ فإنَّما التَّصفيق للنِّساء]   رواه البخاري ومسلم]

 

[Atakayepatwa na jambo ndani ya swala yake na aseme: Sub-haanallah,ama kupiga makofi ni kwa wanawake]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

7. Kumfunguza Imamu anapo sahau katika kisomo

Amepokea  Ibnu Umar radhi za Allah ziwe juu yake Asema Mtume aliswali swala na akasoma akachangana(kisomo) alipo maliza akamuliza Ubayyah je uliswali pamoja na sisi?? akasema ndio akamwambia: Ni nini kilikuzuia? (Kunirekebisha nilipo changaya kisomo)      [Imepokewa na Abuu Daud na Isnadi yake ni Hasan]

8. Kuashiria kwa Mkono kwa ajili ya kurudisha salamu

Amepokea Ibnu Umar radhi za Allah ziwe juu yake asema nilimuliza Bilal  Mtume akirudisha vipi salamu anaposwalimiwa akiwa katika swala? akasema (Bilal) alikuwa akiashiria kwa mkono wake.     [Imepokewa na Abuu Daud na At Tirmidhiy]

9. Kutoa ishara ya kufahamisha kwa anae swali wakati akitokewa na haja

10. Kumshukuru Mwenyezi Mungu anapoona linalo kupelekea kufanya hivyo

11. Kutema mate na kohozi katika Swala upande wakushoto

12. Kumzuia anaepita mbele ya mwenye kuswali

Kwa kauli ya Bwana Mtume :

 

إذا كان أحَدُكم يُصلِّي، فلا يدَعْ أحدًا يمرُّ بين يدَيْه، ولْيَدرأه - (يعني ليدفعه) - ما استطاع، فإنْ أبَى فلْيُقاتله؛ فإنَّما هو شيطان

 

[Atakaposwali mmjoa wenu kuelekea kitu (kinachomsitiri na watu,) asimuachie mtu kupita mbele yake na amzuie kwa kadri ya uwezo wake, Akikataa basi na amzuie kwa nguvu, kwani huyo ni shetani].     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Kwa ujumla inafaa kufanya kila tendo ambalo halipingani na adabu, suna au unyenyekevu wa swala. Kama vile mtu kujikuna na kadhalika, isipokuwa tu anafaa kufanya haya tulioeleza kwa Dharura anapokuwa na haja ya kufanya hivyo.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487208
TodayToday314
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 49

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5ab82a64f10914339581735285432
title_676e5ab82a74a19795092731735285432
title_676e5ab82a8473187796501735285432

NISHATI ZA OFISI

title_676e5ab82bff616632213481735285432
title_676e5ab82c0eb18362659641735285432
title_676e5ab82c1de5163565611735285432 Add content here

HUDUMA MPYA

: 13 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com