Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


 

Suali: Ni zipi Fadhla za Swala?

Jawabu: Swala ina Fadhla nyingi Miongoni mwa fadhla zake ni hizi:

1. Swala ni nuru kwa mwenye kuswali. Mtume ﷺ amesema:

 

 والصلاة نور]       رواه مسلم] 

 

[Na Swala ni Nuru]       [ Imepokewa na Muslim.].

 

2. Swala ni kafara ya dhambi. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema:

 

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ}       هود:114}

 

[Na simamisha Swala ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zinazokaribiana na mchana. Hakika mema yanafuta maovu. Hayo ni makumbusho kwa wenye kukumbuka]      [11: 114].

 

Na amesema Mtume ﷺ:

 

رَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ، هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ؟  ، قَالُوا: لَا يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ، قَالَ:  فَذَلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، يَمْحُو اللهُ بِهِنَّ الْخَطَايَا      رواه البخاري ومسلم

[Mnaonaje, lau kuna mto mlangoni mwa mmoja wenu ambao anaoga ndani yake kila siku mara tano, je kutasalia chochote cha uchafu mwilini mwakeWakasema: Hakutasalia uchafu wowote katika mwili wake. Akasema Mtume ﷺ: Huo ndio mfano wa Swala tano,. Mwenyezi Mungu kwa hizo Swala anayafuta madhambi]   [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

 

3. Swala ni sababu ya mtu kuingia Peponi. Mtume alimwambia Rabi’ah bin Ka’ab, alipomtaka wasuhubiane naye Peponi,: Mtume akamjibu:

 

 فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ ، بِكَثْرَةِ السُّجُودِ ]    رواه مسلم]

 

[Nisaidie kwa kuishughulisha nafsi yako kwa kusujudu sana]     [Imepokewa na Muslim.].


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7887004
TodayToday137
Highest 05-20-2026 : 12580
US
Guests 45

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6a3b7e959ce6f9877584291782283925
title_6a3b7e959cebe19484289481782283925
title_6a3b7e959cf0a5794112041782283925

NISHATI ZA OFISI

title_6a3b7e959d4938580967271782283925
title_6a3b7e959d4d63393487901782283925
title_6a3b7e959d52117340439961782283925 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com