Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suali: Nipi hukumu ya swala tano?

Jawabu:  Swala tano ni wajibu kwa kila Muislamu, kulingana na Qur'ani, na Sunna na umoja wa wanavyuoni:

1. katika Qur’ani:

Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ}    البقرة:43}

 

[Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wenye kurukuu]      [Al-Baqara: 43].

Na Amesema tena katika aya nyingine:

 

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا}    النساء:103}

 

[Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu]    [Al-Nnisaai:103]

2. Na katika Sunna:

 

بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان       رواه البخاري ومسلم 

 

Amesema ﷺ:[Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: kushuhudia kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na mtume wake, na kusimamisha Swala, nakutoa Zaka, nakuhiji Alkaba na kufunga mwezi wa Ramadhani] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na imepokewa kutoka kwa Twalhah bin ‘Ubeidillah kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume kuhusu Uislamu, akasema :

 

خمسُ صلواتٍ في اليوم واللَّيلة]، فقال هل عليَّ غيرها؟ قال: [لا، إلاَّ أن تَطوَّع]   رواه البخاري ومسلم]

 

[Ni Swala tano mchana na usiku. Akasema: “Je, kuna nyingine zinazonilazimu sizizokuwa hizo?” Akasema: La, isipokuwa ukijitolea]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Umoja wa wanavyuoni:

Umma kwa umoja wao wamekubaliana juu ya uwajibu wa Swala tano kipindi cha mchana na usiku,na kuwafikiana bila ya khitilafu yoyote kwamba swala ni mojawapo ya nguzo za Uislamu.

SWALA INAMLAZIMU NANI?

Swala inamlazimu kila Muislamu, aliyebaleghe, mwenye akili, awe mwanamume au mwanamke.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6573205
TodayToday1272
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 28

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828805165f2c14425291671747484753
title_682880516609220070414281747484753
title_68288051661f620077692031747484753

NISHATI ZA OFISI

title_6828805172bb817862585991747484753
title_6828805172c9f19696253711747484753
title_6828805172d752060209851747484753 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com