Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


ALAMA ZA LAYLATUL QADR

1. Ni usiku ambao hauna joto wala baridi kali.
Kutoka kwa Jaabir ibn Abdillahi radhi za Allah ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume ﷺ:

 

إني كنتُ أريتُ ليلة القدر ثم نَسيتُها وهي في العشر الأواخر، وهي طلقة بلجة لا حارة ولا باردة]    رواه إبن خزيمة]

 

[Nilikuwa nimeoneshwa Lailatu Al-qadr, kisha nikasahaulishwa, nayo iko katika nyakati za usiku wa kumi la mwisho, nao ni usiku wenye bashasha unang’ara usio na joto wala baridi]     [Imepokewa na Ibnu Khuzeymah].

2. Jua linatokeza Asubuhi yake jeupe halina Miale.
Anasema Ubeyi ibn Ka’ab radhi za Allah ziwe juu yake alipoulizwa kuhusu dalili za Lailatu Al-qadr:

 

وأمارتها أن تطلع الشمس في صبيحة يومِها بيضاء لا شعاع لها]      رواه إبن حبان]

 

[Na dalili yake ni kuchomoza kwa jua asubuhi yake likiwa leupe halina miale]. [Imepokewa na Ibnu Hibbaan]

Na katika upokezi wa Muslim: [Jeupe halina miale].

MAELEZO
1. Ni juu ya kila muislamu kuzidisha kufanaya ibada katika siku kumi za mwisho za mwezi wa ramadhani kwa sampuli ya ibada mbali mbali kwa sababu ni masiku bora ya mwaka.

2. Ni juu ya Muislamu asipoteze wakati wake katika masiku matukufu na msimu wa kheri kwa kufanya upuzi na mchezo na kuzurura masokoni, na kutembea sehemu zisizo kuwa nahaja.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

8355461
TodayToday577
Highest 09-30-2026 : 21356
US
Guests 54

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6ac8e6db03d478096302351791551195
title_6ac8e6db03d9910411215271791551195
title_6ac8e6db03de614520932811791551195

NISHATI ZA OFISI

title_6ac8e6db197a316637245751791551195
title_6ac8e6db1981921137480851791551195
title_6ac8e6db198849399344381791551195 Add content here

HUDUMA MPYA

: 7 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

Go to top
UongofuUongofu.com