SOMO LA FIQHI
Mambo yanayo pendekezwa kufanywa ndani ya Laylatul Qadr
1. Kufanya itikafu
Nayo ni katika kumi lote wala sio usiku wa Lailatu Al-qadr peke yake, kutoka wa A’isha radhi za Allah ziwe juu yake anasema:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعْتَكِفُ الْعَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ] رواه البخاري ومسلم]
[Alikuwa Mtume ﷺ akifanya itikafu katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
2. Kusimama usiku wake hali yakuamini na kutaraji malipo
Amesema Mtume ﷺ:
مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ] رواه البخاري ومسلم]
[Atakayesimama usiku wa Lailatu Al-qadr hali ya kuwa na imani na kuridhia, husamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Kuomba Dua:
Kutoka kwa A’isha Allah awe naye radhi Anasema:
يا رَسُولَ اللهِ، أرَأيْتَ إنْ عَلِمْتُ أيُّ لَيْلَةٍ لَيْلَةُ الْقَدْرِ، مَا أقُولُ فِيها؟ قَالَ: قُولي: اللَّهُمَّ إنَّكَ عَفُوٌّ كَرِيمٌ تُحِبُّ العَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي] رواه الترمذي]
[Nilisema: Ewe Mtume wa Allah, ikiniafikia Lailatu Al-qadr niombe kitu gani? Akasema: Sema: Ewe Mola! Hakika yako wewe ni mwenye kusamehe (madhambi) tena Mkarimu wapenda sana kusamehe, basi nisamehe (makosa yangu)] [Imepokewa na Tirmidhi.].
4. Kuwaamsha watu wa nymbani kwa ajiliya ibaada
Amepokeya bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake Amesema:
كَانَ النبي - صلى الله عليه وسلم - إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ شَدَّ مِئْزَرَهُ، وَأَحْيَا لَيْلَهُ، وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ] رواه البخاري]
[Alikuwa Mtume ﷺ likiingia kumi la mwisho akijifunga kibwebwe na akikesha usiku wake na akiamsha wake zake] [Imepokewa na Bukhari.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.