SOMO LA FIQHI
Mpangilio wa Matendo katika Siku ya Iddi
Sunna katika mipangilio ya siku ya idd ni kama inavo fuata:
1.Kutupa vijiwe.
2. Kuchinja.
3. Kunyoa au kupunguza.
4. Kufanya Twawafu.
5. Kufanya sai kwa mwenye sai,
Na lau atatanguliza moja katika mambo haya juu ya jengine yafaa na hakuna ubaya wowote, kwa sababu Mtume ﷺ Aliruhusu hilo, lau mtu atanyoa kwanza kisha akatupa mawe itasihi, na lau atachinja kwanza kisha akafanya Twawafu kisha akatupa vijiwe ni sawa, kwa sababu hakulizwa Mtume ﷺ kwa mwenye kutanguliza jambo na kuakhirisha jengine ila akisema:
افْعَلْ وَلاَ حَرَجَ] متفق عليه]
[Fanya na hakuna ubaya] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Kuhalalishiwa Mara ya Kwanza na Kuhalalishiwa Mara ya Pili:-
Kuhalalishiwa ya kwanza:
Ni kuhalalishiwa yote yale yalokuwa ni haramu kufanya kwa mwenye kuwa katika ihram isipokuwa kufanya tendo la ndoa au kufunga ndoa itakuwa si halali kwake kufanya hivyo, na inapatikana mtu kuhalalishiwa kwa kufanya mawili katika yanao fuata:
kutupa vijiwe kwenye jamaraat, kunyoa au kupunguza, kufanya Twawafu pamoja nakufanya sai kwa atake kuwa na sai
Kuhalalishiwa mara ya pili:
Ni kuhalalishiwa kufanya yote yale yaliokuwa ameharamishiwa kufanya alipokuwa kwenye ihram, na hupatikana uhalali wapili kwa kufanya yale yalio tangulia yote pamoja.
- Kuchinja haina mafungamano na kuhalalishiwa, lau atachelewesha kuchinja mpaka siku ya pili siku ya kumi na moja, na akafanya yale mengine siku ya idd atakuwa amehalalishwa.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.