Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Aliye kwenye ihramu akisumukwa na Nywele tatu anapopangusa kichwa katika kutawadha au kuoga, hilo halimdhuru. Pia lau baadhi ya nywele za masharubu au ndevu zilisumuka au ukucha wake ukakatika, hilo halitamdhuru, isipokuwa akizisumua kwa kusudi. Na mwanamke analingana na mwanamume katika hilo la kutodhurika na kusumukwa na nywele au kucha.

Inafaa kwa aliye kwenye ihramu kufunga uzi mguuni mwake akihitajia hilo au kukiwa na maslahi ya kufanya hivyo.

UWEKAJI MASHARTI KATIKA NIA 

Ambaye ni mgonjwa, au anaogopea kutokewa na jambo lenye kumzuia kukamilisha ibada yake ya Hijja, ni sunna kwake aweke sharti wakati wa kuhirimia na aseme:

 

[لبيك عمرة، أو لبيك حجاً، "فإن حبسني حابس فمحلي حيث حبستني]

 

«Tunaitikia mwito wako wa Umra (au Hija) iwapo kutatokea kitu chochote chenye kunifunga mimi (nisimalize ibada yangu,) basi mahali pangu pa kutahalali ni pale uliponifunga».

Bibi Aishah radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliingia kwa Dhuba'ah binti Zubair akamwambia: (Huenda ulitaka kuhiji) Aksema: “Najikuta naumwa. Akamwambia:

 

حجي واشترطي وقولي : اللهم محلي حيث حبستني]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Hiji na ujiwekee sharti na useme ‘ Ewe Mola! Mahali pangu pa kujifungua na ihramu ni pale uliponifunga]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Akisema hivyo, kisha akapatikana na jambo la kumzuia, basi itafaa atahalali (ajifungue na ihramu) bila kulazimiwa na kitu.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7887009
TodayToday142
Highest 05-20-2026 : 12580
US
Guests 65

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6a3b7f7504f0411479876261782284149
title_6a3b7f7504f5414708864581782284149
title_6a3b7f7504fa24249122071782284149

NISHATI ZA OFISI

title_6a3b7f750552b855925241782284149
title_6a3b7f750557711211827231782284149
title_6a3b7f75055c11860654351782284149 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 6 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com