Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Muislamu Akiazimia kusafiri kwenda hija au umra ni lazima afuate muongozo yanayo fuata:

1. Ausie jamaa zake na watu wake kumcha mwenyezi mungu, nako ni kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake.

2. Aandike watu anowadai na wanao mdai na ashuhudishe juu ya hilo

3. Afanye haraka kutubia twaba iliyo yakweli kutokamana na madhambi yote Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا}    التحريم:8}

 

[Enyi Mulio amini tubuni kwa Mwenyezi mungu Toba iliyo ya kweli ]    [ATtahriim: 8]

4. Ikiwa atakuwa na dhuluma za watu kutokana na nafsi au mali au hishima awaregeshee wenyewe au awaombe msamaha kabla ya hajasafiri, kama ilivyo sihi kutoka kwa Mtume

 

من كانت عنده مظلمة لأخيه من عرضه أو من شيء فليتحلله منه اليوم قبل أن لا يكون دينار ولا درهم إن كان له عمل صالح أخذ منه بقدر مظلمته وإن لم يكن له حسنات أخذ من سيئات صاحبه فحمل عليه

[Yoyote atake kuwa na dhuluma ya ndugu yake kutokamana na mali au hishama amuombe msamaha hapa duniani kabla yakutofaa dinari na dirhamu: ikiwa atakuwa na amali njema yatachukuliwa apewe Yule alie mdhulumu, na ikiwa hana mema yatachukuliwa maofu ya mwenzake abandikwe yeye]  [Imepokewa na Bukhari.]

5. achague katika mali yake mali ya halali ya kuendea hijja au umra Amesema Mtume ﷺ:

 

إن الله طيِّبٌ لا يقبل إلا طيبًا]     رواه مسلم]

 

[Hakika Mwenyezi mungu ni Mzuri hakubali ila kizuri]   [Imepokewa na Muslim.]

6. Akusudie hijja yake au umra yake Radhi ya Mwenyezi Mungu na Nyumba ya akhera na kujikurubisha kwake kwa linalo mridhisha Mwenyezi Mungu kutokamana na maneno na vitendo na atahadhari sana kukusudia hija yake mambo yakidunia kama kutaka kusifiwa na kujifakhiri kwa hilo.

7. Na yatakikana kwa mwenye kutaka kwenda hijja au umra kujifunza mambo muhimu yatakao kuifanya hija yake kuwa sahihi, kwa kuuliza asilo lijuwa na kuondosha mushkili, ili afanye ibada yake akiwa mjuzi, na jambo lakusikitisha ni kuwa baadhi ya watu wanaenda hija au umra bila ya kujifunza hukumu zake na kufanya mambo yenye kuharibu hija zao bila kujua.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6573500
TodayToday1567
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 25

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68289977788188764356541747491191
title_682899777890218384501911747491191
title_68289977789e59654174151747491191

NISHATI ZA OFISI

title_6828997779fc55514371591747491191
title_682899777a0a619636796871747491191
title_682899777a1829442749331747491191 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 14 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com