AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Katika aya za mwanzo zilizoshuka, ndani yake mlikuwa na Amri ya Swala; Muqatil bin Suleiman amesema: "Mwenyezi Mungu ﷻ Alifaradhisha Sala mwanzoni mwa Uislamu, na ilikuwa na rakaa mbili tu zilizokuwa zikisaliwa jioni. Kutokana na Kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ :
وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ} غافر:55}
[Na umtukuze Mola wako na kumsifu jioni na asubuhi] [40:55]
Ibn Hajar amesema, "Kuwa kabla ya Mtume ﷺ kupelekwa mbinguni, alikuwa akisali kwa kupunguza na vile vile masahaba zake. Hakuna uhakika kama kilifaradhishwa kitu kabla ya Sala tano au hapana. Inasemwa kuwa faradhi hiyo ilikuwa ni Sala kusaliwa kabla ya machweo na baada ya mawio."
Al-Harith bin Usama amepokea kutoka kwa Ibni Luhay'a mapokezi hayo yakiwa yameungwa kutoka kwa Zaid bin Harith, ya kuwa katika mwanzo wa kupewa Wahyi, Jibril (a.s) alimtokea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ na akamfundisha namna ya kutawadha ... Ibn Maja naye pia amepokea maneno ambayo yana maana hiyo, na umepokelewa mfano wa maneno hayo kutoka kwa Al-Baraa bin 'Aazib na Ibn 'Abbas, na katika upokezi wa Ibn 'Abbas inasemwa: "Na liiikuuia hilo ni jambo la mwanzo kufaradhishwa (1)
Ibni Hisham amesema, "Wakati waSala ulipoingia Mtume ﷺ na masahaba wake walikuwa wakienda nyuma ya majabali na kujificha ili waswali bila ya kuonekana na jamaa zao. Kwa hakika iko siku Abu Twalib alimwona Mtume ﷺ na Ali (r.a.) wanasali na akawauliza kuhusu jambo hilo. Alipoelewa ukweli wa jambo lenyewe aliwaamrisha kulidhibiti na kudumu nalo." (2) *
1) Mukhtasar Siraiu Rrasul, Uk.88.
2) lbn His/Jam, Juzuu 1, Uk. 248.
* Ar Raheeq Al Makhtum 121-122
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.