AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Abubakar (r.a) Aliposilimu akaanza harakati za kufikisha wito wa Uislamu, yeye alikuwa ni mtu aliyezoeleka, mwenye kupendwa, mwepesi, aliyekuwa na tabia nzuri. Jamaa zake walikuwa wakienda kwake kutokana na elimu yake ya biashara na mapenzi yake kwa watu. Alimwita kila aliyemuamini na kumtegemea katika watu wa karibu yake, na wale waliokuwa wakienda na kukaa naye.Walioingia katika Uislamu kwa ulinganio wake ni,Uthman bin Affan Al-Umawi
Az-Zubair bin 'Awwam AI- Asadi
Abdulrahman bin 'Auf
Sa'ad bin Abi Waqqas Al- Zahryan
Twalha bin 'Ubaydullah AI- Tiymy
hawa watu wanane ndio waliowatangulia wengine baada ya watu kutoka katika nyumba ya Mtume ﷺ.
Waislamu wengine wa mwanzo ni Bilal bin Rabah al- Habashi,
kisha akawafuatia hao muaminifu wa Umma huu, Abu Ubayda 'Amir bin Al-Jarrah kutoka katika ukoo wa Banu AI-Harithi bin Fihri.
Kisha wakafuatia, Abu Salima bin Abdil Assad, na AI-Arqam bin Abi AI-Arqam, wote wawili wakitoka katika ukoo wa Makhzoum.
'Uthman bin Madhoun na ndugu zake wawili, Qadama na Abdullah, Ubaydah bin Al-Harithi bin Al-Muttwalib bin Abdi Manafi, Saeed bin Zaid Al-Adawy na mke wake Fatuma binti Al-Khattab Al-Adawiyya, dada yake Umar bin Al-Khattab, Khabbab bin Al-Aratti na Abdullah bin Masoud Al-Hudhali na watu wengine waliowafuata, nao pia wakawa ni miongoni mwa watu wa mwanzo. Hawa wanatoka katika koo zote za Kikureishi.
Ibni Hisham aliwahesabu zaidi ya watu arubaini.P? na aliwataja baadhi yao kuwa walikuwa watu wa mwanzo ingawaje wanazuoni wanatofautiana kidogo katika hilo. Ibni Ishaq anasema, "Kisha wakaingia watu katika Uislamu makundi kwa makundi, Wanaume na Wanawake. Kwa njia hiyo utajo wa Uislamu ukaenea katika mji wa Makka na ukawa unazungumziwa." (1)
Hawa wote waliingia katika Uislamu kwa njia ya siri na Mtume ﷺ alikuwa akikutana nao na kuwaongoza kwenye Dini kwa kujificha, kwa sababu Da'wa ilikuwa bado ni kwa mtu mmoja mmoja. Wakati huo Wahyi ulikuwa ukifuatana.
Baada ya kushuka kwa aya za mwanzo za Surai AI-Muddathir, aya na vipande vya sura zilizokuwa zikishuka wakati huo zilikuwa fupi fupi, zenye vituo vyenye kuvutia, vyenye mipaka na mvuto wa sauti iliyo tulivu yenye kuvutia inayowiana na mazingira hayo ya ukimya yaliyo mepesi. Aya hizo zilikuwa zimekusanya mafunzo ya utakasaji wa nafsi, na kufahamisha ubaya wa kuzichafua nafsi na tope la dunia. Zikawa zikiisifu pepo na moto kana kwamba viwili hivyo viko katika macho ya watu, zikawapeleka waumini katika anga jingine tofauti na anga ambalo jamii ilikuwa inaishi wakati huo.*
(1) Sahihil Bukhari, Mnnaqib Ab" 'Llbaidah Bin Al-larrah, [uzuu 1, Uk. 530.
127 lbn His/mm, Juzuu 1, Uk. 245-262.
* Arraheeq Al Makhtum 120-121
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.