AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Hawa ndio watu katika kundi ambalo linajulikana katika historia ya Uislamu kuwa ndio Waislamu wa mwanzo, wakiongozwa na mke wa Mtume ﷺ, mama wa waumini Bi Khadija binti Khuwailid,
kijana wake Zaid bin Haritha bin Sharahbiyl AI-Kafuy,
mtoto wa ammi yake Ali bin Abi Twalib, wakati huo akiwa bado mtoto mdogo akiishi katika ulezi wa Mtume ﷺ ,
na rafiki yake mpenzi Abubakar (r.a). Hawa walisilimu katika siku ya kwanza ya Da'wa kwa watu katika Dini.
Kwa hivyo wa Kwanza Aliesilimu katika wanaume ni Abubakar Swiddiq (r.a)
na katika Wanawake ni Bibi Khadija bint Khuwailid (r.a).
na katika watoto ni Ali bin Abi Twalib (r.a).
na katika vijakazi ni Zaid bin Harith (r.a).
* Ar-Raheeq Al Makhtum 119
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.