Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


MAKHTUUM


MIAKA MITATU YA DA'WA YA SIRI

Inaeleweka kuwa Makka ilikuwa ndio kituo cha Waarabu. Walikuwapo waangalizi wa Al-Ka'aba, na waangalizi wa masanamu yaliyokuwa matakatifu mbele ya Waarabu wote. Kwa sababu hiyo, kazi ya kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa katika kufanya matengenezo hapo Makka ilikuwa ni kazi pevu iliyokuwa na ugumu wake na matatizo mengine makubwa kabisa. Jambo hilo lilihitaji uimara na azma isiyoyumbishwa. 

Matukio ya misiba na majanga ilikuwa ni katika hekima na busara mbele ya mazingira kama hayo. Katika siku za mwanzo Da'wa ilifanywa kwa njia za siri, ili kuepuka kuzusha mgogoro na watu wa Makka, kwa mafundisho ambayo kwa hali yoyote ile yangewacharura. 

Kundi la Kwanza
Lilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mtume .   kuutangaza Uislamu kwa watu waliokuwa karibu naye kwanza, kwa kuanzia nyumbani kwake na kwa marafiki zake wa karibu. Kwa hivyo aliwaita kwenye Uislamu na alimwita kwenye Uislamu kila ambaye aliiona kheri kwake, miongoni mwa wale anaofahamiana nao, aliokuwa anawajua kwa Kumpenda Mwenyezi Mungu .

Kwa vile wengi wao walikuwa wanafahamu alivyokuwa mkweli, jinsi alivyokuwa mpenda kheri, na alivyo mwema, walimuitikia. Watu hao hawakuwa na shaka yoyote kwa ukubwa wa jukumu alilopewa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu , utukufu wa nafsi yake na ukweli wa khabari yake.


* Ar-Raheeq Al Makhtum 118-119


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668022
TodayToday710
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 12

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_686694ca9b75916565373161751553226
title_686694ca9b83a8671383051751553226
title_686694ca9b91010505901751553226

NISHATI ZA OFISI

title_686694ca9ceca14034352851751553226
title_686694ca9cfa68478615741751553226
title_686694ca9d07e15764738281751553226 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 4 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com