AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Inawezekana kuzigawa nyakati za Da'uia (wito) ya Mtume ﷺ kwenye vipindi viwili vilivyo kamilika kama ifuatavyo:
1). Kipindi cha Makka
kilichochukua takriban miaka kumi na mitatu.
2). Kipindi cha Madina
kilichochukuwa takriban miaka kumi kamili.
Kila kimoja katika vipindi hivyo viwili vinakusanya awamu; kila awamu ina mambo ya pekee yaliyokuwa tofauti na mambo ya awamu nyingine, na hilo limedhihiri, baada ya uchunguzi wa kina katika mazingira ambayo Da'wa yalipitia katika vipindi hivyo viwili. Tunaweza kukigawa kipindi cha Makka katika awamu tatu.
(1). Awamu ya Da'wa ya siri, miaka mitatu.
(2). Awamu ya kutangaza Da'wa kwa watu wa Makka tokea mwanzoni mwa mwaka wa nne wa Utume, mpaka mwisho mwa mwaka wa kumi.
(3). Awamu ya Da'wa nje ya Makka, tokea mwisho wa mwaka wa kumi wa Utume mpaka kuhama kwake Mtume ﷺ kuelekea Madina.
Ufafanuzi na Awamu ya Madina utaelezwa peke yake.*
* Ar-Raheeq Al Makhtum 117
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.