Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


 shaier Untitled 1jhjhhh


Mtume alipokea amri nyingi kwa Kauli Zake Mwenyezi Mungu

 

{يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ قُمْ فَأَنذِرْ  وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ  وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ  وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ  وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ  وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ}

 

[Ewe uUyejifunika maguo!, Simama uonye (viumbe). Na Mola wako umtukuze, Na nguo zako uzisafishe. Na mabaya yapuuze, (endelea kuyapuuza). Wala usiwafanyie ihsani (viumbe) ili upate kujikithirishia (wewe hapa duniani). Na kwa ajili ya Mola wako fanya subira (kwa kila yatakayokufika]. " [74:1-7] 


Haya ni maamrisho mepesi ya kawaida katika mtazamo wa nje, lakini yenye maana kubwa kabisa katika lengo lake, na yaliyo na nguvu katika athari zake kwa kuhamasisha vitendo katika uhakika wa mambo na uhalisi wake: 

1. Kikomo cha kusimamia uonyaji ni kuwa asiachwe mtu yeyote katika wale wanaokhalifu amri na kwenda kinyume na yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu wa viumbe, isipokuwa awe ameonywa na Adhabu Zake Allah , nampaka utokee mtikisiko wa tetemeko katika moyo wake. 

2. Lengo la Kumtukuza Mwenyezi Mungu  ni kuwa kusiwepo na mkubwa yeyote katika ardhi, isipokuwa ajue kuwa uwezo wake utavunjwa, utapinduliwa 'nje ndani na kuangamizwa usibaki katika ardhi isipokuwa Ukubwa wa Mwenyezi Mungu Aliye Mtukufu. 

3. Lengo la kuzisafisha nguo na kuyaepuka masanamu ni kutufikisha katika kusafisha sehemu ya nje na ya ndani. Kutufikisha pia katika kuitakasa nafsi na takataka zote na uchafu wote mpaka kufikia kiwango cha mwisho cha ukamilifu. Ukamilifu unaowezwa kufikiwa na nafsi ya mwanaadamu chini ya kivuli cha Rehema za Mwenyezi Mungu Zilizokienea kila kitu, Hifadhi Yake, Ulinzi Wake, Mwongozo Wake na Nuru Yake. Mpaka awe ni mfano wa juu katika jamii ya wanaadamu, ili zivutike Kwake nyoyo zilizosalimika, na nyoyo zilizopotoka kuhisi Ukubwa Wake, mpaka idhihirike kwake dunia yote kwa kupatana au kutofautiana. 

4. Lengo la kutotaka ziada kwa kutoa, ni kumuasa kuwa asivihesabu vitendo vyake na jitihada zake kuwa ni mambo makubwa sana. Lakini pia asiache kuwa anajitahidi katika kutenda mema, kufanya juhudi na kujitoa muhanga. Kisha ayasahau yote hayo na azingatie zaidi kupata Radhi za Mwenyezi Mungu , kwa sifa ya kuwa hatayahisi yale ambayo ameyatoa na kuyafanya. 

5. Katika aya ya mwisho, pana ishara kwenye yale ambayo yalimtokea, katika kumpinga, kumcheza shere, kumkejeli, kufanya juhudi za kutaka kumwua, kuwaua masahaba wake, pamoja na kutaka kuwaangamiza waumini waliotaka kujitinga naye. Mwenyezi Mungu Alikuwa Akimwamrisha kusubiri kwa yote hayo, kwa uvumilivu na kwa ajili ya kupata radhi za Allah. 

Mwenyezi Mungu ni Mkubwa. Ni Wepesi ulioje wa maamrisho haya katika sura yake ya nje, na uzuri ulioje katika kuathiri kwake kulikotulizana kwenye kuvutia. Ubora na uzito ulioje katika utendaji wa kuzichambua pepo kali zenye kuvuma kwa kasi zinazokusanya pande zote za ulimwengu na kuziunganisha baadhi yake na baadhi. *


*Ar-Raheeq Al Makhtum 112-113

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785144
TodayToday145
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 32

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a952b9b751c6713458781755927225
title_68a952b9b760514911660261755927225
title_68a952b9b76f316474188071755927225

NISHATI ZA OFISI

title_68a952b9b8c8f15090971461755927225
title_68a952b9b8d7213283904381755927225
title_68a952b9b8e5b5790996361755927225 Add content here

HUDUMA MPYA

: 14 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com