AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Kabla hatujaingia kufafanua kipindi cha ujumbe na Utume, tunaona kuwa ni bora kwanza tukaelewa hatua za Wahyi ambao ndio chimbuko la Ujumbe na msingi wa maudhui ya Da' awa.
Ibnu -Qayyim alipokuwa anazitaja hatua za wahyi alisema:
1. Kudhihiri kwa ndoto za kweli, ilikuwa mwanzo wa Wahyi kwa Mtume ﷺ
2. Kwa yale ambayo Malaika alikuwa akiyapenyeza kwenye fikra na moyo wake, bila ya yeye kumwona, kama alivyothibitisha hilo Mtume mwenyewe ﷺ kwa kusema,
إنّ رُوحَ القُدُسِ نَفَثَ في رُوعِي أنّ نَفْساً لنْ تَمُوتَ حَتّى تَسْتَكْمِلَ أجَلَها وَتَسْتَوْعِبَ رِزْقَها، فاتّقُوا الله وأجْمِلُوا في الطَّلبِ، ولا يَحْمِلنَّ أحَدَكُمُ اسْتِبْطاءُ الرِّزْقِ أنْ يَطْلُبَهُ بِمَعْصِيَةِ الله، فإنّ الله تعالى لا يُنالُ ما عِنْدَهُ إلاّ بِطاعَتِهِ. رواه أبو نعيم في حلية الأولياء وصححه الألباني.
[Kwa hakika Roho Mtakatifu - Jibril (a.s) - amepulizia katika moyo wangu ya kuwa, haitakufa nafsi yoyote mpaka ikamilishe riziki yake, kwa hiyo mcheni Mwenyezi Mungu (s.w.t) na tafuieni riziki zenu katika njia za halali, na wala kuiafuta riziki isiwe ndiyo sababu ya kumuasi Mwenyezi Mzmgu ﷻ kwani vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ﷻ hauipatikani isipokuwa kwa Kumtii Yeye.]
3. Ngazi nyingine ilikuwa ni kwa Malaika kujidhihirisha kwake katika sura ya mwanaadamu, ambaye alisema naye mpaka alipoyazingatia yale yaliyokusudiwa kwake, na katika ngazi hii mara nyingi masahaba walikuwa wakimwona.
4. Ngazi nyingine ilikuwa ni kwa Mtume ﷺ kujiwa na wahyi kwa mfano wa mlio wa kengele uliokuwa na kishindo, hapo alivaana na Malaika mpaka paji lake la uso likamiminika jasho katika siku yenye joto kali. Kama alitokewa na hali hiyo akiwa amepanda mnyama kama farasi au ngamia, ilikuwa ni lazima mnyama huyo apige magoti kwa utukufu na uzito wa tukio l enyewe.
Kwa hakika inahadithiwa kuwa ipo siku alijiwa na Wahyi katika hali hiyo, hali ya kuwa paja lake likiwa juu ya paja la Zaid, likawa zito juu yake kiasi cha kukaribia kulivunja.
5. Ngazi nyingine ni ile ambayo Mtume ﷺ alikuwa akimwona Malaika katika sura yake halisi aliyoumbwa nayo, na humfunulia yale ambayo Mwenyezi Mungu ﷻAmeyataka Ayafunue. Hali hii ilitokea mara mbili katika kipindi chote cha Utume kama alivyolitaja hilo Mwenyezi Mungu ﷻkatika Surat An-Najm (Sura ya 53).
6. Ngazi nyingine ni yale Aliyomfunulia Mwenyezi Mungu ﷻ wakati Alipompandisha Mbinguni usiku wa Miiraji na kumfaradhishia Sala na Kumpa mengineyo Aliyompa.
7. Ngazi nyingine ni maneno ya Mwenyezi Mungu ﷻ kwa Mtumeﷺ moja kwa moja kutoka Kwake, bila ya kupitia kwa Malaika, kama vile ambavyo Mwenyezi Munguﷻ Alivyozungumza na Nabii Musa bin Imran (a.s). Ngazi hii imethibitika kwa Musa moja kwa moja, kwa maelezo ya Qur'ani. Kuthibiti kwake kwa Mtume wetu Muhammad ﷺ ni katika usiku wa Isra'.
Wanawazuoni wa somo la Sira wameongeza nyingine, nayo ni Mwenyezi Mungu ﷻ Kumsemesha kwa uwazi bila ya kuwepo kwa pazia yoyote, na haya ni mas' ala ambayo yana tofauti kati ya wanawazuoni waliotangulia na wale wa sasa. Huu ni muhtasari mfupi katika kuweka wazi ngazi mbalimbali katika upokeaji wa Wahyi,(1)
Ukweli ni kuwa hii ngazi yarnwisho haikuthibitishwa. *
(1) Zaadul Ma'ad, Uk. 18.
* Ar-Raheeq Al Makhtum 109-111
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.