AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Ibni Hajar anasema: 'Kukatika kwa Wahyi kulikuwa kumekusudiwa kumuandaa Mtume ﷺ na kumuondoa khofu aliyokuwa nayo, na ili ipatikane shauku ya kurejea huo wahyi.(1)
Baada ya kuondoka kwa vivuli vya kuoteshwa na zikathibiti alama za uhakika na Mtume ﷺ akajua kwa yakini kuwa amekuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Aliye Mkuu na Mtukufu, na kuwa aliyemjia ni Mjumbe wa mbinguni aliyetumwa kumletea khabari kutoka kwa Mwenyezi Mungu ﷺ. Ikawa kutazamia kwake kuja kwa Wahyi ni sababu ya kuongezeka yakini; na uvumilivu wake ni maandalizi ya Wahyi kurejea. Jibril alimjia kwa mara ya pili. Bukhari amepokea kutoka kwa Jabir bin Abdillahi, kuwa yeye alimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akizungurnzia kukatika kwa wahyi: "Wakati ninakuienda, ghafla nilisikia sa uti kutoka mbinguni nikanyanyua macho yangu na kutazama mbinguni, nikamwona Malaika ambaye alinijia kaiika pango la Hiraa amekaa juu ya kiti, katikati ya mbingu na ardhi, nikapiga magoti na kuporomoka mpaka kwenye ardhi, niliposimama nikarudi nyumbani ninatetemeka. Nikisema, 'Nifunikeni, Nifunikeni, wakanifunika, na hapo Mwenyezi Mungu ﷺ Akateremsha Sura:
{يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ قُمْ فَأَنذِرْ وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ}
[Ewe Uliyejifunika maguo. Simama uonye (viumbe). Na Mola wako umtukuze. Na nguo zako uzisafishe. Na mabaya yapuuze.] [Al-Muddaththir:1-5]
kisha Wahyi ukawa unakuja kwa nguvu,' mfululizo na
kufuatana.(2) *
1) Fathul Bari, Juzuu 1, Uk. 27.
2) Sahihil Bukhari, Kitab Ttafsir, Babu Rrijz Fahjur, [uzuu 2, Uk. 733.]
*Arraheeq Al Makhtum 108
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.