SIMULIO LA BIBI AISHA KATIKA KUTEREMKA KWA WAHYI
Hebu tumsikilize Aisha mtoto wa Abubakar Siddiq radhi za Allah ziwe juu yake akitueleza kisa cha tukio hili ambalo Iilikuwa ni mwenge wa Nuru ya Mwenyezi Mungu ﷺ, ulioanza kuondoa weusi wa giza la ukafiri na upotevu mpaka ukabadilisha mapito ya maisha, na kusahihisha barabara ya Historia.
Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema jambo la kwanza ambalo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ alianza kuletewa katika wahyi ni ndoto za kweli akiwa usingizini, ikawa haoti ndoto yoyote isipokuwa huja kutokea mtano wa mwangaza wa asubuhi. Baada ya" hapo akapendelea "zaidi kukaa . faragha katika pango la Jabal Hiraa, akawa anafanya ibada zake masiku kadhaa kabla ya kurudi kwa watuwaKe, kila alipotaka kurudi tena alikuwa akijiandaa kwa ajili ya faragha hiyo, mpaka ilipomjia haki wakati akiwa ndani ya pango la Jabal Hiraa. Alitokewa na Malaika aliyemwambia: "Soma!", naye akajibu; "Mimi sijui kusoma:' Amesema: "Akanikamata na kumminya sana kisha akaniachia nakuniambia tena: Soma, nikamjibu tena: Mimi siiui kusoma"; Akaniminya tena kwa mara ya tatu, akaniachia 'na kuniambia:
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ
[Soma kwa jina la Mola uiako Aliyeumba. Amemuumba muianadamu kwa pande la damu. Soma, na Mola wako Karimu sana.] [96:1-3]
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alirejea na Aya hizo hali ya kuwa anatetemeka kwa woga,' akaingia .nyumbani' kwa Khadija binti Khuwaylidi na kumwambia:
زملوني زملوني
'Nifunikeni,nifutiikeni, wakamfunika mpaka alipoondokuia na khofu aliyokuwa nayo: Baadaye, Khadija radhi za Allah ziwe juu yake alimwuliza, nimepatwa na nini? akamweleza habari, Kwa hakika nilihofia nafsi yangu.
Bi Khadija radhi za Allah ziwe juu yake akamueleza:
[كلا والله ما يخزيك الله أبدا ، إنك لتصل الرحم وتحمل الكل وتكسب المعدوم وتقري الضيف وتعين على نوائب]
"Wewe si mtu wa kuwa na khofu. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), hatokudhalilisha milele. Kwa hakika wewe unaunga udugu na unabeba.uzito wa wanyonge, unasaidia masikini, unakirimu wageni, na unasaidia katika matatizo ya kweli.
* Arraheeq Al Makhtoom 102-103
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.